Wakwepe marafiki wanafiki, ikiwezekana waambie ukweli

Wakwepe marafiki wanafiki, ikiwezekana waambie ukweli

Jack Daniel

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2021
Posts
2,912
Reaction score
12,904
Salaam jamiiforum.

Kila siku zinavyozidi kwenda ndivyo ambavyo huwa tunajuana na watu mbalimbali, tukikutana safarini,mikutanoni, sehemu za ibada na maeneo mengi.

Watu hawa baada ya kufahamiana au kujuana kwetu wapo ambao hugeuka kuwa watu wa karibu na kutengeneza bond ama urafiki fulani.

Lakini baadaye zipo tabia ambazo huwa zinajitokeza Kwa huyo unayemwita rafiki yako ,kama hizi,

1.Kupenda ofa zako sana.

Si mara moja ,ni mara nyingi unamuita rafiki yako mnakunywa,mnakula na kufurahi pamoja. lakini yeye hafanyi hivyo au anakupigia simu na kukuuliza, leo wapi? Unamjibu huna kitu huku ukimtaka kama yupo vizuri mkafurahi Kwa bili zake.anakujibu hana kitu , lakini baada ya muda unapata taarifa kuwa anakula Raha na watu wengine.muepuke.

2.Kupenda kuazima ikiwa yeye ni mchoyo.

Kila akikutangazia kakwama ,unamuokoa lakini wewe hata ukwame Tatizo la shilingi Mia moja ya kitanzania hawezi kukupa ,yeye kila siku hana tu.muepuke.

3.Mkosoaji kupita kiasi.

Kukosolewa si kubaya ni njia ya kukurudisha kwenye mstari.lakini mtu mwenye kukosoa kila kitu chako huyo siyo mtu mzuri sana ,watu mia wameona uko sawa yeye tu kaona upo tofauti.muepuke

4. Mwenye wivu

Unamuita rafiki yako,lakini ukimuonesha nyumba uliyojenga,biashara yako au mradi uliofungua kisha anabadilika na kuonesha chuki ya wazi ni balaa.
Umejibana umeamua kununua simu ya gharama kuendana na features nzuri, halafu utasikia mbona umenunua simu ya gharama Sana ikipotea? Huoni ni hasara? Mimi siwezi hiiihii inanitosha.muepuke.

5.Mwenye kufanya mipango yake kimya kimya.

Unamwita rafiki yako,miradi yako unamuonesha
Safari zako unamuaga,na hata Siri zako kumwambia,ila yeye ni kinyume chake mipango yake utaisikia Kwa watu tu,muepuke.

6.Mwenye kupenda kusema watu wakiwa hawapo.

Mpo watatu kwenye maongezi yenu,mmoja akitoka Tu,kununua vocha au sigara,kashamuongelea vibaya tena vitu visivyo vya lazima au mambo yasiyowahusu.

7.Mwenye kutamani mpenzi wako.

(Hapa siongelei mke)

Katika stori zenu na huyo ,rafiki yako mnayeitana mwana,ukamsimulia habari za demu fulani kuwa ulipiga,basi naye anafanya mpango mpango naye akapige. huyo muepuke

8.Mwenye kupenda sifa na kujionesha kama anazo.

Rafiki huyu hafai,hafai ,hafai.mpo zenu mahali mnapiga kilevi mara anajisifia,au kukusifia kuwa anazo pesa,huyu muda wowote anaweza kukuponza.
Mtu mwenye kuonesha Mali zako Kwa watu wa kila aina pengine lengo lake siyo Baya huyo muonye aache.

9.Mwenye kudharau wengine.

Mtu huyu si rafiki mzuri,huenda amejenga urafiki na wewe kisa cheo chako,Mali zako na ushawishi wako,siku ukidrop ,hutomuona tena.

10.Mgomvi ,mtu mtata.

Huyo rafiki yako ambaye anaanzisha utata ,haishi vizuri na majirani,mkiwa kwenye starehe anaanzisha timbwili,kisa wewe rafiki yake ni afisa wa jeshi au kitengo kwahiyo anaonea watu Kwa kukutegemea wewe kama kinga yake , muepuke na mchane laivu

11.Mtu mdhalilidhaji,

Wewe ni rafiki yake ndiyo,lakini kisa ana uwezo juu kipesa,cheo na wadhifa ndiyo akukosoe mbele za watu,au kutweza utu wako mbele za mademu ili kutafuta sifa. ananunua kitu kisha anakupa ufunguo ukaweke kwenye gari huo ni udhalilishaji.labda kama umekubali kudhalikika.

Yapo mengi tu/yanafanywa na marafiki zetu hatupendezwi nayo na tunaona aibu kuwaambia Kwa kuona mtavunja urafiki wenu.jiepusheni na matatizo kabla hayajawafika.

Chukua yanayokufaa.
 
Back
Top Bottom