Wala mihogo wajaribu kuupandisha thamani muhogo ili waishi kwenye thamani hiyo

Wala mihogo wajaribu kuupandisha thamani muhogo ili waishi kwenye thamani hiyo

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,017
Reaction score
5,294
Akili ya binadamu ni kitu cha kushangaza.

Mtu anaweza kuchukia sana kwa kuitwa na mpenzi wake kiazi kitamu, lakini mtu yule yule akiitwa sweet potato na mpenzi anaweza kujiona yuko mawinguni kwa raha kama zote.Kumbe tafsiri ya kitu ndiyo tatizo.

Mtu huchukia akiambiwa neno kutokana na tafsiri ya hilo neno na jinsi anavyoichukulia. Hawa watu wa utopolo waliambiwa wala mihogo wengi walichukia sana, ijapo huo ndio ukweli. Hata hivyo walichukuia sana kwa kuwa licha ya wao kuonekana mchango wao kwa yanga ni kula mihogo tu, bado wanaamini wamekuwa na mchango mkubwa kwa timu yao usioonekana moja kwa moja na unaoonekana wazi.

Nimefurahi tu kwa hatua ya wao kuupa thamani muhogo na kusema unauzwa masaki. Watu wanapanga foleni kununua muhogo coco beach.
Wanasema kwa sasa muhogo unauzwa hoteli kubwa za Dar. Kwa hiyo muhogo ni chakula cha hadhi.

Baada ya kuupandisha thamani, nadhani sasa hata sisi wengine tukiwaita wala mihogo, haitakuwa tusi tena
 
Back
Top Bottom