Walalamika wajawazito kujifungua kwenye majaruba ya mpunga

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Wananchi wa Kijiji cha Mwashagi Kata ya Lyabukande Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, wamelalamikia ubovu wa miundombinu ya barabara na ukosefu wa Zahanati unaopelekea wajawazito kujifungulia kwenye majaruba ya mpunga."

Wamedai kuwa tatizo hilo limekuwa likiwakabili hasa kwenye kipindi cha msimu wa mvua, kuwa barabara hua hazipitiki kwenda kufuata huduma ya afya makao makuu ya Kata umbari wa zaidi ya kilomita tano, na kusababisha wajawazito kuanguka kwenye majaruba ya mpunga na wengine kujifungulia humo humo.

Wananchi wa kijiji hicho walipaza sauti zao juzi wakati Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, alipofanya ziara kijijini humo kukagua utekelezaji wa mradi wa majisafi na salama, ambao umekamilika kwa asilimia 98 na umeshaanza kutoa huduma ya maji.

Mmoja wa wananchi hao Maguta Jilili, amesema wanaipongeza Serikali kwa kuwapelekea huduma hiyo ya majisafi na salama, lakini bado wanakabiliwa na tatizo kubwa la ubovu wa miundombinu ya barabara na hata kusababisha wajawazito kujifungua kwenye majaruba kipindi cha msimu wa mvua.

“Mvua zikinyesha barabara kwenye kijiji hiki hazipitiki na hata wewe Mkuu wa wilaya umejionea mwenyewe, inatulazimu kupita juu ya kingo za majaruba, tabu inakuja kwa wajawazito namna ya kupita na wengine huangukiano na kujifungua,” amesema Jilili.

Nao wanawake wa Kijiji hicho akiwamo Mbaru Minza, wamesema wamekuwa wakipata tabu kupata huduma ya kujifungua na kuiomba Serikali kuwa karabatia miundombinu ya barabara pamoja na kuwajengea Zahanati ili waipate huduma hiyo karibu.

Naye diwani wa Lyabukande Luhende Kawiza, amekiri kijiji hicho kukabiliwa na ubovu wa barabara na kubainisha kuwa tatizo hilo alishaliwasilisha kwenye vikao vya baraza la madiwani.

Akizungumzia ukosefu wa zahanati, amesema amesha hamasisha wananchi kijiji humo kuanza kuijenga na sasa ipo hatua ya msingi ambayo wataijenga hadi hatua ya Renta, na kubainisha katika bajeti ya mwaka wa fedha (2023-2024) wataiombea fedha ili Serikali iikamilishe na kuanza kutoa huduma.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, amesema tayari alishaagiza Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA), kukarabati miundombinu ya barabara kijijini humo, huku akiwapongeza wananchi kwa kujitoa kuchangia shughuli za maendeleo, ikiwamo kuanza kujenga Zahanati kwa nguvu zao.

Chanzo: Nipashe
 
Kwani mwigulu wao anasemaje, hahaaaa nacheka utadhani mazuri
 
daah ktk miaka zaidi ya60 ya uhuru.Shame
 
Back
Top Bottom