Lakini kuna wengine Wanasema kuoana ni kufanana, Je unalizungumziaje hili? Na Kama ni sawa, unafikiri ni sawa kwa wanandoa kulitimia neno hili na labda kuna mbadala?!Kuoana ni neno lenye maana ya kupatana, wakati kuoa ni kupata na kuolewa ni kupatwa. Watu mume na mke hatusemi Fulani kapata na Fulani kapatwa kwamaana ya kuoa na kuolewa bali tunasema wamepatana kwamaana ya kuoana. TUKI 2014 wanafasili neno "oa" kuwa ni kufanya muungano na mwanamke ili kukaa pamoja naye kama mke na mime kulingana na sheria, mila, desturi au taratibu za ndoa za mahali panapohusika.
Barafu la moto
Ndio, kuoana inaweza kuwa kufanana. Muktadha ndio unaoukiria kilongo cha kutumika, kwalugha nyepesi ni sawa na kusema neno oa/ oana huwa na maana kwakutegemea na mazingira ya utumizi wake. Mfano katika mitihani ya kiswahili tunatumia neno oanisha ikiwa na maana fananisha/ linganisha/ patanisha/ n.k. lakini kwa muktadha wa ndoa sio sahihi kulifasili neno oa kwakusema ni kufanana, kwenye ndoa linaweza kufasiliwa kama kukubaliana kuishi pamoja(kupatana), kuungana, n.k. Ingawa katika jamii za kiafrika hatutumii msamiati wa kuoana bali wa kuo na kuolewa tu, hili ni kutokana na utamaduni wa mwanaume kumlipia mwanamke na kumhudumia.Lakini kuna wengine Wanasema kuoana ni kufanana, Je unalizungumziaje hili? Na Kama ni sawa, unafikiri ni sawa kwa wanandoa kulitimia neno hili na labda kuna mbadala?!
Sent using Jamii Forums mobile app
Sijui kwa taratibu nyingine lakini nijuavyo kwenye Uislamu mume anaoa na mke anaolewa sio kuoana