Wale tulio na dhamira ya kuvuta jiko kwa majirani zetu tupeane mbinu za hapa na pale!

Baba Mama

Senior Member
Joined
Apr 1, 2018
Posts
107
Reaction score
138
Ngoja kwanza nishushe darasa, ili dhamira yetu ieleweke vema zaidi.

'No offence' kwa wanawake wetu wa kibongo. Hakika ni warembo sana kimwili na kitabia.

Lakini kwa mustakabali wa kimaendeleo ya kitaifa, kuna baadhi ya kaka zenu ama wadogo zenu tumeona ni hekima kubwa sana kufanya ile wazungu wanaita 'diversity state' kwa ajili ya kuchochea fikra bora na hatimaye maendeleo ya Taifa.

Tazama mfano wa 'diversity' ya USA na kwa hapa Africa tazama South Africa. Hakika, kuna jambo la kujifunza sana kwenye maendeleo yao kitaifa na mtu mmoja mmoja kwenye hayo mataifa. Hadi hapo nadhani tupo pamoja.

Ukweli, ulio dhahiri ni kwamba fikra zetu wenyewe km watz zimefeli 'big time' katika kila kitu. Sisi wananchi wa kawaida pamoja na viongozi wetu tumekwama kwa kila kitu. Pumzi zimekata kabisa. Hatuna tena mbinu mbadala kwa ajili ya kuendeleza Taifa letu. Sisi maisha yetu yamekuwa 'bora kunakucha'.

Sasa sisi wachache, tumeona kuwa, mbinu mbadala ni kuchanganya 'race' za mataifa mbalimbali ndani ya nchi yetu kwa akili ya kuchochea fikra chanya na maendeleo ya Taifa letu. USA na SA ni case study ya kutosha.

Hivyo basi, kama Ali Kiba alivyoungana na wabongo wenzie kwenye kujenga 'diversity state' nasi tupo nyuma yake tunakuja. Diamond japo kazingua lkn at least kazaa nae sio mbaya sana.

Hivyo, tukutane hapa tupeane mbinu mbalimbali za hapa na pale kwa ajili ya ku win situations katika dhamira hii.

Kipekee, naomba kumwalika member mwenzetu Sky Eclat kwa ajili mchango wake wa experience za hapa na pale.

Ladies and gentlemen karibuni sana tukomboe Taifa letu.
 
Teh teh ngoja nami niende burundi ni karibu na home hata kwa kuogelea nafika πŸ˜€πŸ˜€
 
Shukran mkuu, kwanza kuoa au kuolewa unaenda kwa msukumo wa moyo. Si kuwa Tanzania tumefeli la hasha mbona huku kwetu tunacheza harusi kila siku unakuta bwana harusi ni wa Temeke amekuja kuoa Kwamtogole.

Raha za kuoa au kuolewa na foreigner ni kuwa mke anakuja kuanza maisha mapya, ile michepuko yako kabla ya ndoa wala atakua haijui na kama si mtu wa kupenda umbea wala hatakaa aijue.
Mapishi utapikiwa maharage tu lakini viungo ni vingine kiasi unavchanganyikiwa.

Changamoto ni kuwa, mke au mume akikimbia na watoto inabidi utafute passport kwenda kuwafuata. Wakati wangekimbilia Kigoma ungeunganisha tu mabasi mpaka unafika.
 
Yeah, umeelezea kwa angle nyingine zaidi enewei sio mbaya. Sisi hatuoi wale vichwa ngumu wasiojielewa km yule wa Emmanuel Eboue, hapana. Tunaoa watu wanaoeleweka, maana lengo ni kusaidia Taifa liwe na 'diversity' ya kuridhisha.
 
Updates:
Za kunyapianyapia zinasema kuwa huko Congo wabongo tunakubalika sana.

Kuna Zambia , Zimbabwe, Burundi, Rwanda, Mozambique, tunakubalika sana. Mwenyewe wanatuona sisi wa ushuani hahaha wao wanajiona wapo porini. So, hii ni added advantage.

Malengo yetu ni kuwa kufikia 2030 walau Taifa lina mchanganyiko mkubwa wa karibu nchi zote jirani na sisi.

Tukifanikiwa maana yake nchi jirani tutakuwa tunakwenda vile tutakavyo maana tayari tuna connections si tumeoa kwao? So, maisha yanaanza kuwa mtelezo kwa vijana wetu fursa kibao yaani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…