Wale tuliowahi kuwa na wapenzi wasiojua kusoma na kuandika tukutane hapa

Wale tuliowahi kuwa na wapenzi wasiojua kusoma na kuandika tukutane hapa

Craig

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2013
Posts
1,512
Reaction score
2,712
Habari za majukumu wadau, ni matumaini yangu kuwa wote tumeonesha uzalendo kwa kushiriki vizuri zoezi la sensa 2022.

Dodoso za sensa zimenifanya nikumbuke visa nilivyowahi kukutana navyo kwenye mahusiano. Ilikuwa mwaka 2010 enzi hizo nilikuwa naishi Masaki, Haille Selassie Road(nyumbani). Nyumba ya jirani yetu ilipangishwa, kutokana na ujirani mwema nilikuwa na mazoea na wakazi wa nyumba hiyo ambayo walipanga wachina, akiishi mkurugenzi wa mradi mkubwa wa barabara.

Sasa walikuwa na pisi moja kali ya kihaya(Kokunyumisa) kama chief cooker. Toto jeusii tii, bonge la guu, msambwanda upo, limepanda hewani, linaongea kichina na kingereza kizurii. Basi mzee mzima nikajipendekeza pisi ikanizoea nikatema sumu likanielewa tukaanzaa mahusiano.

Sasaa mpenzi wangu huyo hakuwahi kunitumia sms hata siku moja yeye ni kupiga tu, hata nikituma sms nipo bize job nitext yeye ni kupiga tuu. Chale zikanicheza baada ya mwezi huyu atakuwa illiterate?! Siku moja moja nikashika simu yakee kuingia kwa sms hakuna hata sms moja zaidi ya zile za networks provider na promotions.

Nikaendelea kuuchuna kadri anavyonizoea akawa ananiambia nimsomee sms zake kimasikhara mimi nikawa nimeshang'amua huyu demu ni ngumbaruu. Tuliendelea na mahusiano nikajifanya sijui. Basi nilikuwa kama sekretari wake maana hata kufanya miamala yake ya banking na simu nilifanya mimi, na demu alikuwa akiwapiga wachina dollars zao walizoshinda kwenye kamali.

Tulikuja kuachana mkataba wa Wachina ulipoisha akarudi kwao Kagera, nilimpenda sana. Kama na wewe uliwahi kukutana na kisa kama hiki tiririka.

Craig kwa sasa Kigoma.
 
Jf imevamiwa. Nyuzi hizi ulaya wachangiaji wengi
 
Mimi nina jamaa yangu sio mpenzi mambo yafuatayo yalinifanya nijue hajui kusoma wala kuandika;

1. Kwenye Mpesa anasimama mbali umsaidie utasikia tu password 2000.Ukimuita hasogei hata kwa kifaru.
2. Kuunga mabando anakutupia tu vocha utasikia niunge cha wiki jombaa.
3. SMS ikiingia kama uko karibu anakurushia simu huku akicheka haaa haaa msikie huyo anasemaje
4. Ukimtext anakupigia tuuu.

Ila smart sana msafiii maneno mengi.
 
Wengi wasojua kusoma wanakua wajanja hao balaa kwenye simu,ukibip kapiga fastaa yaani,wanakariri namba za watu kichwani mnoo!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mimi nina jamaa yangu sio mpenzi mambo yafuatayo yalinifanya nijue hajui kusoma wala kuandika;

1. Kwenye Mpesa anasimama mbali umsaidie utasikia tu password 2000.Ukimuita hasogei hata kwa kifaru.
2. Kuunga mabando anakutupia tu vocha utasikia niunge cha wiki jombaa.
3. SMS ikiingia kama uko karibu anakurushia simu huku akicheka haaa haaa msikie huyo anasemaje
4. Ukimtext anakupigia tuuu.

Ila smart sana msafiii maneno mengi.
Nimecheka kwa sauti yaaani mambo haya
 
  • Thanks
Reactions: EEX
Back
Top Bottom