Kichwamoto
JF-Expert Member
- Jan 21, 2019
- 3,403
- 4,692
Napenda hivyo na huwa nakwepa uongozi kabisa.Hautapata nafasi ya uongozi hata siku moja. Tegemea kuongozwa hadi siku unaingia kaburini.
napenda hivo na huwa nakwepa uongozi kbsa.
Sio kwa mimi baharia ambae ni multidisciplinary by nature, low profile but an average Don as per my dimensions based on global indicators.Utakufa masikini... na mshahara wa laki 5 kwa mwezi kabla ya makato.
Vipi huwa unadeclare interests kuondoa mgongano kimaslahi wa mchango wako?Sijawahi kuwa kimya yaani SIJAWAHI.
Kuna kikao kilikuwa ni sisi Vs Wizara mbili.
Yaani nilifunguka mpaka mkuu wangu akawa anatuma sms Kuni-mind.
Kukaa kimya huku Kuna madudu SIWEZI
#YNWA
Duu,husinikumbushe ndugu yangu,nilishawahi kuuliza swali moja kwenye kikao fulani cha bodi swali ambalo halikuwa nyuma ya mpango (listed)nikaleta mtafaruku wa pata shika nguo kuchanika sitasahau;ILIKUWA HIVI;Kuna mashirika fulani uwa yanambelewa na bodi ya kurungezi kuongea na WATUMISHI aidha mara moja kwa mwaka au mara mbili,sasa kutokana na viongozi husika kutojiamini uwa wanahisi kuna vichwa vinaweza kuuliza maswali yenye HATARI;Sasa,kabla ya bodi kufika wiki moja kabla mnaitwa watumishi wote halafu kila mmoja anauliza swali ambalo anahisi ataiuliza bodi hata kama ni la kijinga,maswali yenye utata yanapanguliwa yasiyo kuwa na utata wanapangwa watu maalum/kuaminika watakaouliza bila kuongeza nyongeza nje ya swali husika.Sasa bodi husika ikifika,mkurungezi husika anamwiita mkuu wa kituo husika kumuuliza maswali yatakayoulizwa ambayo naye pia hayatamletea shida anayapitia,endapo mkurungezi akiona kuna swali ambalo lina walakini basi yule aliyepangwa kuuliza swali anapewa kazi ya ghafla au safari ya ghafla yenye maslahi kwake aidha posho nk ili hasiudhurie kikao bila yy kujua.Asalaam wanajf!
Binafsi huwa napata wakati mgumu kwenye vikao maeneo mbali mbali hasa kwa tahadhari ya kupunguza negative people. Huwa natafakari faida na hasara za kuchangia ama kutochangia maoni kuhusu jumbo husika. Natulia kimya nafuatilia kwa umakini nachukua notes ila natumia code za kilatini.
Nikilazamishwa naomba udhuru dakiika 2 mbili short call, nikirudi natumia Kimemia principle what others had to say, naafiki maamuzi ya kikao ndio imetoka hio.
Nahamia kwenye kanuni na miongozo zigo kwa mwenyekiti
Vipi nyie wengine mnalinda vipi interests au Image zenu?
Note;Kama hizi vikao za bado zipogo nadhani bodi zikitembelea mashirika husika ziache mtindo wa kupenda kuulizwa maswali ya wazi hayana afya kabisa na ni hatari kwa watumishi hasa wauliza maswali na wajue wakiendelea hivi wajue wanabebaga masuali feki yasiyo na faida kwa watumishi wa chini bali huficha uovu wa wakuu hisika eneo la kazi kwani yanakuwa yamepangwa.Mimi napendekeza Mwenyekiti wa bodi atoe nafasi ya kuandika maswali ya siri kwenye vikaratasi halafu yasomwe hadharani,aisee bodi itatoka na vitu vitamu hatari sana na ndo msaada wa watumishi wa chiniDuu,husinikumbushe ndugu yangu,nilishawahi kuuliza swali moja kwenye kikao fulani cha bodi swali ambalo halikuwa nyuma ya mpango (listed)nikaleta mtafaruku wa pata shika nguo kuchanika sitasahau;ILIKUWA HIVI;Kuna mashirika fulani uwa yanambelewa na bodi ya kurungezi kuongea na WATUMISHI aidha mara moja kwa mwaka au mara mbili,sasa kutokana na viongozi husika kutojiamini uwa wanahisi kuna vichwa vinaweza kuuliza maswali yenye HATARI;Sasa,kabla ya bodi kufika wiki moja kabla mnaitwa watumishi wote halafu kila mmoja anauliza swali ambalo anahisi ataiuliza bodi hata kama ni la kijinga,maswali yenye utata yanapanguliwa yasiyo kuwa na utata wanapangwa watu maalum/kuaminika watakaouliza bila kuongeza nyongeza nje ya swali husika.Sasa bodi husika ikifika,mkurungezi husika anamwiita mkuu wa kituo husika kumuuliza maswali yatakayoulizwa ambayo naye pia hayatamletea shida anayapitia,endapo mkurungezi akiona kuna swali ambalo lina walakini basi yule aliyepangwa kuuliza swali anapewa kazi ya ghafla au safari ya ghafla yenye maslahi kwake aidha posho nk ili hasiudhurie kikao bila yy kujua.
KIMBEMBE;Mie nikajifanya kiburi kwani hii tabia ilishanikera kitambo ya kuona maswali yetu ya msingi yanaminywa kila mwaka,bodi ikiondoka matatizo yanaendelea,so kwenye kikao cha awali mimi nilimute sikuuliza lolote,sasa bodi imekuja,mwenye bodi yake (Mkurungezi mkuu),utaratibu wa maswali feki na wauliza feki ukaanza na kuisha,sasa ili mkurungezi kujiaminisha/kujifanya hasitiliwe shaka na bodi akatoa nafasi ya kipekee ambayo mimi kichwa maji kenge nilikuwa naisubiri[emoji23][emoji23][emoji23].Akasema"nadhani huu ndo mwisho wa maswali yetu,au kuna mwingine ana swali la nyongeza?"Mimi,mkono na kidole juu wima!!!!Aisee,Mkurungezi, mkuu wa kituo,watumishi wenzangu halafu nilikuwa nimekaa nyuma kwenye kona wote waligeuka na kunitumbulia mimicho!!!Mie nshaweka K vant ndogo kichwani ya kujihami make nilijua kifatacho ITV; nikakomaa na swali langu,bodi ikachukua note muhimu;
Ila kilichonipata baada ya bodi kuondoka,nilijuta kuzaliwa.Make hilo swali lilileta ukakasi wa HATARI, toka hapo sijawahi kuuliza au kutoa maoni yoyote katika kikao chochote na sitarudia hata km ni kikao cha Sungusungu mtaani kwangu.