Wale wa Bwiru Boys: Tukumbushane maisha na mikasa ya Bwiru

Wale wa Bwiru Boys: Tukumbushane maisha na mikasa ya Bwiru

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,515
Reaction score
28,506
Nakumbuka maisha ya Bwiru Boys miaka hiyo ilikuwa full mikasa.

Kulikuwa na eneo linaloitwa Mombasa, mahali ambapo vijana wa Boys walikuwa wanazama kuwapiga chabo mabinti wa girls pindi wanaoga.
Sehemu hii ilikuwa maarufu sana maana upande wa Ziwa waiokuwa wanautumia wasichana wa Girls maarufu kama "mende" ulikuwa unatenganishwa na upande wa boys kwa kilima fulani hivi kina mawe ya hatari, lakini vijana walikuwa wana risk life kwenda kula chabo.

Nakumbuka ishu ya headmaster wetu kupindi hicho kulikuwa na tetesi kuwa anapita na mistress wa Nganza, sasa kimbembe kilikuwa ole wenu siku ya debate au bugi(disko) mtoe pendekezo la kuwaleta Bwiru Girls, headmaster ataahirisha hata hilo disko, ila mkimletea mabinti wake wa Nganza, hata usafiri atawapa free.

Nakumbuka misemo maarufu kama kuguga likimaanisha kupiga msuli au kusoma, msemo kama kugenya likimaanisha kufariki, msemo kama fororo ukimaanisha uji usio na sukari, msemo kama mnyambo ukimaanisha mtu mwenye tabia za ubaguzi na kujisikia sikia , msemo kama kudabo ukimaanisha kudrudia msosi mara mbili, form one wakiitwa nguruwe na mingineyo mingi.

Nakumbuka pia visa vya mwanafunzi mmoja alikuwa shombe shombe alikuwa bingwa wa kupita na wake za maticha, mpaka akazaa na mke wa ticha mmoja hivi(Jina tunalihifadhi), akazaa kijana shombe shombe na kuleta mtikisiko mkubwa sana kwenye ndoa ya ticha wetu.

Walimu kama Mazebele, Rung'wecha, Begenyeza, Kissuu, Mchizi Mox, Massaba(R.I.P), Ruhiye(R.I.P) na wengineo wengi.

Nasikia pia kuwa hata Founder wa Forum hii muheshimiwa sana Maxence Mello ni product ya Luthuli Domitory pale njia ya kuelekea ukarani na alikuwa ngugi kweli kweli(just kidding).

Tukumbushane life ya Bwiru aisee.

12651326_10201448336607019_3786303634314722495_n.jpg
 
Hahahaha!! Nakumbuka siku mmepewa kisago baada ya kufanya kituko cha mwaka...Kipindi kile mashine za kupump maji zimezingua.
Ha ha ha kituko gani??
Nakumbuka kituko tulichofanya ni vijana kununua petroli kwenda kumchoma mlinzi wa pump ya maji anaitwa handsome baada ya kuwabania vijana waliokuwa wametorosha wabanti girls na kuwapeleka ufukweni kula bata.

Zaidi ya hapo hatujawahi kupewa kisago aiseee
Sie tulikuwa watata sana miaka yetu sie.
 
Yap, maeneo ya mnarani. Mwanzo mwa term tulikua tunajazana kule kula ubwabwa wa mgole
He he he he
Umenikumbusha mbali sana mkuu.

Enzi hizo ubwabwa ili kuula ilibidi uwe na kibali kutoka kwa daktari kinaitwa "special diet".

Maisha yanakwenda kwa kasi sana aiseee.

Mwaka juzi nilikwenda maeneo hayo, nimekuta pameharibika sana, ukarani imevamiwa na matajiri kwa sasa watu wameachia mijengo ya maana, kila mahali kuna fence.
 
Ha ha ha kituko gani??
Nakumbuka kituko tulichofanya ni vijana kununua petroli kwenda kumchoma mlinzi wa pump ya maji anaitwa handsome baada ya kuwabania vijana waliokuwa wametorosha wabanti girls na kuwapeleka ufukweni kula bata.

Zaidi ya hapo hatujawahi kupewa kisago aiseee
Sie tulikuwa watata sana miaka yetu sie.
Nipe range ya mwaka uliokuwepo pale nikwambie ni kituko gani
 
He he he he
Umenikumbusha mbali sana mkuu.

Enzi hizo ubwabwa ili kuula ilibidi uwe na kibali kutoka kwa daktari kinaitwa "special diet".

Maisha yanakwenda kwa kasi sana aiseee.

Mwaka juzi nilikwenda maeneo hayo, nimekuta pameharibika sana, ukarani imevamiwa na matajiri kwa sasa watu wameachia mijengo ya maana, kila mahali kuna fence.
Daah, kitambo sijafika. Mesini siku ya ubwabwa ilikua mchinjo sana. Siku ikiwa zamu ya bweni lako kugawa chakula unatoroka class ili huwahi kuoda
 
Daah, kitambo sijafika. Mesini siku ya ubwabwa ilikua mchinjo sana. Siku ikiwa zamu ya bweni lako kugawa chakula unatoroka class ili huwahi kuoda
Ha ha ha ha
Tulikuwa tunapanga foleni ndefu mpaka inatokezea upende wa milango ya nyuma ile.

Ukiona prefect wa mesini wakati wa kuoda anachunguia chungulia kuangalia foleni unajua tu tayari mchinjo unataka kuanza.
Unapigwa mchinjo wa haja, halafu mpunga wenyewe ukute upepikwa na mzee misana, alivyo fundi wa kupika
Utatamani kulia aiseee

Hatari sana mkuu, huyo misana kuna siku walimtegea kuwa huwa anaiba mchele. Tuliamshwa saa kumi 2 kwenda milimani kumfukuza[emoji23] [emoji23]
 
Na kuna mwalim mmoja tulikua tunamuita machozi ya simba alikua anapita saa 12 kuamsha watu kwa ajili ya mchakamchaka naskia kuna watu walimpiga na yai viza akakoma
 
Hatari sana mkuu, huyo misana kuna siku walimtegea kuwa huwa anaiba mchele. Tuliamshwa saa kumi 2 kwenda milimani kumfukuza[emoji23] [emoji23]
Ha ha ha ha
siku hiyo nilikuwepo mkuu.

Ila japo jamaa alikuwa anaiba kweli ila tulimdhalilisha sana yule mzee.
Haiwezekani kwa kujituma kote kule tumdhalilishe vile, sema basi tena mambo ya mob psychology.

Siku hizi kastaafu tayari.

Unamkumbuka yule mpishi form one??
Unamkumbuka Bandhiho??
Unamkumbuka mnyama Nyemenohi, mzee wa kitambi kikubwa mpaka kinataka kugusa chini??
Unamkumbuka ticha scorpion??
 
Na kuna mwalim mmoja tulikua tunamuita machozi ya simba alikua anapita saa 12 kuamsha watu kwa ajili ya mchakamchaka naskia kuna watu walimpiga na yai viza akakoma
Ha ha ha ha
yap yule ticha namkumbuka sana, Kanifundisha Brickwork and Masonry yule.
Mpaka nikalamba banda.

Siku hizi yuko Musoma Tech, amechoka sana.
Kawa mlevi wa gongo kupindukia, na anastua kwenye vile vilabu vya uswazi tu.
Nimekutana naye mara kibao.
 
Mwalimu Kiandiki alikua na mtoto mzuri sana, unamkumbuka? I wish ningekua mkubwa kama sasa
 
Back
Top Bottom