Wale wa Kristu wenzangu ni wangapi bado mnamkataa shetani na mambo yake yote?

Wale wa Kristu wenzangu ni wangapi bado mnamkataa shetani na mambo yake yote?

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Wale ambao mlibatizwa mkiwa wadogo, mlipata mafundisho ya dini, mlipokea sakrament zote za kanisa. Wengine mnakumbuka mbuzi wakichunjwa siku ya Kipaimara na watu walikuwa pilau na soda.

Mlimkataa shetani na mambo yake yote lakini
Kanisani hamuendi na wale wanaokwenda wengine hushiriki meza ya bwana baada ya kulala na mchepuko.

Kwenda kwa waganga na kutambikia mizimu.

Kutokusaidia wasio na uwezo tena wengine hukebehi wenye shida.
 
Hata huyo shetani uwezo wa kutenda hayo aliutoa kwa God Hivyo msimlaumu Sana
 
Namkataa shetani na mambo yake yote na kazi zake zote,najitoa kwako ee Mungu baba na mwana na roho mtakatifu ili nikutegemee na kukutumikia kwa uaminifu HATA nitakapokufa.Amen

Hili ungamo nalikumbuka mpaka kesho na najitahidi kuishi katika njia inayompendeza Mungu japo kiubinadamu kuna kukosea(tukisema hatuna dhambi tunajidanganya wenyewe) lakini kiimani baada ya kutubu huwa tunaamini tumesamehewa
 
Bado tupo Mkuu...

Tulimkataa kwa imani ya wazazi wetu tulipokuwa wadogo na tunaendelea kumkataa kwa imani zetu wenyewe tukiwa wakubwa.

Nyakati zote hizo tunafanya hivyo kwa msaada wa Mwenyezi Mungu katika Utatu Mmoja na Mtakatifu pamoja na Mama Kanisa.
 
Wale ambao mlibatizwa mkiwa wadogo, mlipata mafundisho ya dini, mlipokea sakrament zote za kanisa. Wengine mnakumbuka mbuzi wakichunjwa siku ya Kipaumara na watu walikuwa pilau na soda.

Mlimkataa shetani na mambo yake yote lakini
Kanisani hamuendi na wale wanaokwenda wengine hushiriki meza ya bwana baada ya kulala na mchepuko.

Kwenda kwa waganga na kutambikia mizimu.

Kutokusaidia wasio na uwezo tena wengine hukebehi wenye shida.
Mimi hapa.mkristo safi.
Ila nilipata majaribu ya shetani ulipotea jf kama wiki kadhaa tu nikajikuta sina raha.Nimemke m ea dhetani atoke mbali nish as kuwa faza sitako kurudi nyuma
 
Wale ambao mlibatizwa mkiwa wadogo, mlipata mafundisho ya dini, mlipokea sakrament zote za kanisa. Wengine mnakumbuka mbuzi wakichunjwa siku ya Kipaimara na watu walikuwa pilau na soda.

Mlimkataa shetani na mambo yake yote lakini
Kanisani hamuendi na wale wanaokwenda wengine hushiriki meza ya bwana baada ya kulala na mchepuko.

Kwenda kwa waganga na kutambikia mizimu.

Kutokusaidia wasio na uwezo tena wengine hukebehi wenye shida.
Nimecheka eti 'baada ya kulala na mchepuko'

Tulibatizwa bila kujitambua lakini kwa umri huu kama ulizaliwa katika familia ya Kikristo utakuwa umetambua nini yakupasayo kumkataa shetani na mambo yake
Toba na Delivarance ni muhimu
Kwa Father Peter siku ya kitubio hivi Mungu alikuwa anatusamehe kweli ? Hahahhh those days Catholic Church
 
Back
Top Bottom