Wale wa Mbeya Day

Wale wa Mbeya Day

Jibaba Bonge

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2008
Posts
1,246
Reaction score
402
kwa wale waliosoma Mbeya Secondary School (Mbeya Day), Kama mpo humu jamvini hebu tukumbushana kidogo enzi zile. Ile awamu ya kwanza ya vigae na streams mbili 'A' na 'B' kwa form 1&2 na science na commerce kwa form 3&4 na ile awamu ya pili ya baada ya vigae kuondolewa na kuwa bati tupu na streams nyingi kuongezwa na kuanzishwa A level.
I was there from 1980 wakati wa vigae na streams mbili na Headmaster NISAJILE
 
usinikumbushe ule mto unaokatiza nyuma ya mount living stone hotel...
down ze riva...
kulikuwa na mawe tunajificha kule huku tukiota jua.
 
usinikumbushe ule mto unaokatiza nyuma ya mount living stone hotel...
down ze riva...
kulikuwa na mawe tunajificha kule huku tukiota jua.

Ni kweli. na kule kwenye fish ponds upande wa madarasa ya sanaa (wakati huo) tulikuwa tunaota jua sana asubuhi
 
Nakumbuka enzi za Mwl. Mwakas... alitutandika sana viboko. Pia,zile bustani za mboga kule chini karibu na mto.

Pia nakumbuka kulikuwa na stream mbili ABC na LMN. Waliokuwa A na L ni science one.
 
Signature yako ilipatikana katika Uwanja wa Mapinduzi ?? nowadays Sokoine Memorial Stadium
 
Mwandeko
Mwakamele
Mwakasala
Unamkumbuka Mr. Mkwizu. Enzi zile Mr II (Mh. Mbunge) ndo anaanza mambo yake nakumbuka nilikuwa namuona amevaa rozari shingoni. Kulikuwa na rafiki yake Boniface Gwatengile alikuwa mtaalamu sana wa kucheza ''miziki ya wazungu''
 
Nikumbusheni jina la yule mwalimuwa kike wa kiingereza ambaye alikuwa fyatu kidogo na akikukuta unaongea kiingereza utakiona.
 
mmmhh....this is too nanihii I think....kama mumewe ni member wa JF?....too low
Huyu ipo msg anayotaka kuifikisha hapa. Edit post yakoo tuwastue mods watoe hii
 
Duh! kweli maisha ni safari ndefu. Ulipomtaja Mwandeko to nikakumbuka fimbo za matakoni mwezi Juni. Ulipomtaja bwana mdogo Sugu nikakumbuka walikuwa wanacheza shoe siku za graduation. Ila kikubwa ni wali wa mawese tuiokuwa tunakula mchana. Ada ilikuwa sh. 350 kwa mwaka. Duh! tena kuna teacher mmoja wa fine art alikuwa anakigugumizi anaitwa nani vile... ba brother man mmoja eti ndo mwalimu wa typing (Zoya???). sasa hivi shule nzima ni kuta na mageti
 
Whisper,
Yule wa kigugumizi aliitwa Usega kue fine arts. Yule mama Fyatu kidogo jina limenitoka alikuwa anafundisha physics. Je ulikuwepo siku Mch Hiza na dada Lwaga walipotutembelea na Mch. Hiza akaimba nyimbo za Bob Marley. Toka siku hiyo na mimi nikasema ntakuja kuwa mchungaji- msela.

Mwandeko (RIP) alikuwa funny sana yule mzee
 
Nakumbuka Mwandeko alipohamia Mbeya Day alikuwa anatoka Tukuyu asubuhi halafu baada ya kazi anarudi Tukuyu Alifanya hivi kwa miezi mingi tu akitumia basi la KARANJA. Lilikuwa famous sana kwa speed na trip za TKY-MBY-TKY nafikiri ilikuwa mara tatu au nne kwa siku.
 
Namkumbuka na mwal. Mwakyembe Sijui Biology ilimchangaya maana duu alikuwa akifundisha reproduction inakuwa mtafutano!
 
Unamkumbuka mwl wa history Meela au ''Msegeju'' au Mwl wa kiingereza Mr. Mposi na madoido yake ya kugeuza shingo.?

Namkumbuka Magelewenya alivyokuwa mkali wa hesabu, lakini hata yeye alikuwa anamkubali mwanafunzi mmoja akiitwa Nikutusya Mwangupata huyu alikuwa ni balaa kwa hesabu. Mtihani wa form four alipata masomo yote alama C kasoro BAM na Pure Mathetimatics alipata A zote
 
Back
Top Bottom