Wale wa Milambo High School njoo hapa


Duh, 73.? Vipi kipindi hiko.? Watu walikuwa watata.?
 
Milambo imepoa sana aisee 2009 nilikwenda Tabora nikafika mpaka milambo iko tofauti sana na enzi zileeee

Tangu nimemaliza Milambo miaka zaidi ya 20 iliyopita sijabahatika kuitembelea tena shule yangu. Ila iko damuni. Ndiyo iliyonitengeneza nikawa hivi nilivyo leo. Shule ya WANAUME...!!!
 
Duh, 73.? Vipi kipindi hiko.? Watu walikuwa watata.?
Nikwambie Kijana Complex. Milambo tulikuwa wamoja kweli kweli. Tabora Boys/Girls walikuwa nje ya mji hivyo tulikuwa tukiwaita "washamba" Milambo na Kazima ndiyo wa mjini lakini Kazima ilikuwa O level tu hivyo Wazee wa mji tulikuwa siye. Wanasheria wengi nchini wamepita pale. Kaka yake Mhe. Lissu aitwaye Allute sasa wakili A town kapitia pale. Ooh Milambo thanks you are still there. Vijana itunzeni vizuri shule Yetu. Mama Milambo katulea, katutunza, katulisha, katugea elimu bora, ametengeneza majina makubwa nchi hii. Long live Milambo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…