Wale wa old moshi secondary(Moshi sec tujuane hapa)

ketone

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2016
Posts
509
Reaction score
655
Hii shule niliipenda sana nilisoma pale maiaka miwili pale ..nilienjoy kusoma advance mahali pale kwani shule hii ilikuwa na Uhuru wa kutosha..Wengi tulikuwa tunatoroka weekend kucheki mpira pale chuo cha ushirika na hata wengine kwenda kuzamia kwenye sherehe za harusi pale YMCA...

Mabweni tuliishi Mawenzi..kibo...shengena...Sitomsahau headmaster aliyekuwa msomi na mwenye madaha Mr Sanga..baadae Mr angalo..

Darasani physics miaka ile tulipigiwa na msami...mzee huyu alikuwa hacheki na akikupiga fimbo moja ni sawa na umechapwa fimbo tano na mwalimu mwingine.

Chemistry alipiga yule mama nani nimemsahau jina ila vijana walimbatiza quantum..
Mathematics alikuepo Mr kinunda mzee wa shengena..
Biology alikuwepo mzee wa pombe mzee palangyo...
Kipindi hiki watu walilkuwa wanapiga msuli pale darning hall masaa 24 ..
Kama wewe umepitia hapa eleza unachokikumbuka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka gani sasa maana wengine tulipita huko miaka hiyoooooo.

Chuo cha Ushirika ndio tulikuwa tunazamia kupata "special diet" ilikuwa unatakiwa ufanye juu chini uwe na best pale Chuoni unaingia kantini kama na wewe upo Ushirika.

Pia Ushirika tulizamia kuangalia TV, enzi hizo bado Bongo hakuna station ya TV kwa hiyo tunaangalia KBC (Kenya Broadcasting Co operation) na tena ni black and white...siku ya VITIMBI chumba kinajaa mpaka madirishani kuwaangalia kina Masakuu na Maliwaza.

Mita chache kutoka shule kulikuwa na nyumba moja al maarufu kama red house, Masela wakitoka huko wanarudi wanatembelea mikono maana walikuwa wanaandaliwa ile kinywaji haramu isiyo na rangi inayofanana na konyagi.

Kulikuwa na Ticha mmoja anaitwa Mr Temba, huyo alikuwa ni Mdingi mmoja mfupi mnene ana kitambi, huyo kabla hajakuchapa analia kwanza kwa kukusikitikia kinachoenda kukukuta, na kweli ilikuwa fimbo yake moja lazima usikie kizunguzungu.

Kulikuwa na Mwalimu mmoja wa A level, alikuwa anaitwa Mama Luvinga alikuwa ni bonge la kitu...jamaa wakitoka darasani wanakwambia hata hatujamuelwa namna Mama alivyokuwa anarembua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…