Kwa waliosoma sengerema secondary school pekee
chaka bado ipo?
ule uwanja wa basket je??
eti siku hizi mabafu yanatoa maji!!
lile bwawa bado lipo??
mabweni bado yana majina yale yale kama,..mirambo(nililala mimi),kimweri,kibasila,mkwawa
enzi zile disco lilkipigwa bwaloni tulikuwa tunawaalika madem wa nsumba,walipinda kimbwa..
zikifanyika harusi bwaloni,..kadi moja wataingia madenti mia..
namkumbuka nduli,escoba,zungu,gamutu,msavimbi,mchafu,. etc
alikuwepo ticha mmoja anaitwa kachecheba alikuwa nuksi kichizi,pia mwl buga
headmaster alikuwa Matu(RIP),second aliitwa Igosha
alikuwepo ticha mmoja mmarekani alikuwa anavaa nguo wiki tatu bila kuchange
namkumbuka mwita bwaloni,..alikuwa anagawa msosi,akikupiga mnyengo ukilalamika kibakuli anakitupa kule na ugali wake...
nyimbo tulizokuwa tunasikiliza ni za kina tupac,coolio,krisskross,naughty by nature,dabrat,mclyte na wagumu wengine
bongo tuliwasikiliza akina too proud,GWM,Kwanza unit,diplomatz na wengineo
tulikuwa hatuna mobile phones
ilikuwa 1994-1997
na nilikuwa maarufu kwa jina la ORIGINAL GANGSTA(OG),
wewe ni nani na uko wapi