Wale wachezaji Tatu Mzuka mnilijua hili?

Wale wachezaji Tatu Mzuka mnilijua hili?

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
426
Reaction score
685
Hawa jamaa nimewaangalia kwa ukaribu wanavyoendesha bahati nasibu yao. Watu hawa huwa na namba tatu za bahati, kinachonishangaza ni kuwa kila wakati huwapigia simu watu wawili tu wakati wanasema kuwa namba za bahati zinakubalika kwa arrangement yoyote.

Sasa chukulia namba za bahati ni 658, hizi namba zina arrangements sita tofauti
  • 658
  • 685
  • 586
  • 568
  • 856
  • 865
Maana yake ni kuwa kwenye kila droo tunatarajia watu zaidi ya wawili kupigiwa simu ya droo, kutokana na idadi ya arrangemet ya namba ambazo wanazikubali, lakini tangu nianze kuangalia mara nyingi wamekuwa wakiwapigia watu wawili tu na kuwapa pikipiki au milioni moja.

Lakini je, ni kweli kila droo watu wanaopatia namba hizo za bahati wanakuwa wawili tu?

Amkeni, mnaliwa

Signed

Oedipus
 
Watu wa Dar ndo wapenda mteremko. Mtu haoni shida kila siku kutoa jero ili abahatike kuwa milionea siku moja.
 
Nchi hii ulaghai upo sehemu nyingi sana. Acha waliwe.
 
Wenye tamaa acha wapigwe kwa matumaini waliyonayo
 
Kwani kuna great thinkers wa huku nao wanacheza huo mchezo?
 
Back
Top Bottom