Wale wakusema "Tafuta hela, woga wako ndio umaskini wako" wachunguzwe hasa linapokuja suala la watu kupotea kwa utata

Wale wakusema "Tafuta hela, woga wako ndio umaskini wako" wachunguzwe hasa linapokuja suala la watu kupotea kwa utata

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,017
Reaction score
5,294
Nimesikitishwa na jinsi maiti zilivyokutwa kwa mganga wa kienyeji kule Singida.

Hii ni moja ya matokeo ya tamaa kali za mali hasa kwa vijana wa siku hizi wakisukumwa kauli mbiu za kipumbavu zinazoongozwa na visichana na wanawake wasiojielewa.

Tamaa hii kali ya mali na utajiri vimewasukuma wengi kuwa tayari kuua ili kupata hizo pesa wanazotamba nazo.

Kibaya zaidi wapo hadi wachungaji wanaohamasisha mtu atafute hela kwa namna yoyote ili mradi tu asidharauliwe.

Kusema kweli laiti ningekuwa na mamlaka ningepiga marufuku misemo ya kijinga badala yake mtu akikiuka angekamatwa ili alipie gharama.

Tulizoea misemo ya kazi ni kipimo cha utu, fanya kazi, asubuhi kumekucha twende shamba, maisha ni mchezo cheza vizuri fainali uzeeni na mingine yenye kujenga kama heshima ya mtu inatokana na huduma anayoitoa kwa jamii.

Pia soma:
Wanne wakamatwa kwa mauaji ya watu 10 Dodoma na Singida

Kwa sasa inasikitisha misemo ya kishetani imetamalaki na inapakwa mafuta na kusababisha majanga makubwa.
 
Back
Top Bottom