Wale wanaoanza/walioanza biashara (kujiajiri) njooni tujadili kidogo

tajiriboya

Member
Joined
Oct 31, 2019
Posts
15
Reaction score
37
Habarini wakubwa na wale wadogo.

Binafsi baada ya maisha kuwa magumu na kusubiria ajira baada ya muda mrefu bila mafanikio, nimeona nianzishe bishara ya M-Pesa na Tigo Pesa Wilayani Kahama. Niliambiwa na dada yangu kuwa biashara hii inalipa ukiwa makini maana kuna matapeli na wezi pia.

Hii ni siku ya 5 naona wateja wameanza kuzoea, nimeongeza na vocha ili kuongeza huduma. Wale mliokwisha zoea biashara mbalimbali mnaweza kutoa mchango wa mawazo juu ya biashara ambayo mlipitia /mnapitia ili wale ambao walimaliza chuo na bado wako nyumbani wapate mwanga wapi pa kutokea.

Mungu atakuwa na wewe nyakati zote za maamuzi juu ya mustakabali wa maisha yako.
 
Ndiyo natafuta kitambulisho cha Magufuli nianze.
 
Ebu tupe mchanganuo wa maitaji ili nasi tuweze kujikwamua mkuu...
 
Habarini wakubwa na wale wadogo.

Binafsi baada ya maisha kuwa magumu na kusubiria ajira baada ya muda mrefu bila mafanikio, nimeona nianzishe bishara ya M-Pesa na Tigo Pesa Wilayani Kahama. Niliambiwa na dada yangu kuwa biashara hii inalipa ukiwa makini maana kuna matapeli na wezi pia.

Hii ni siku ya 5 naona wateja wameanza kuzoea, nimeongeza na vocha ili kuongeza huduma. Wale mliokwisha zoea biashara mbalimbali mnaweza kutoa mchango wa mawazo juu ya biashara ambayo mlipitia /mnapitia ili wale ambao walimaliza chuo na bado wako nyumbani wapate mwanga wapi pa kutokea.

Mungu atakuwa na wewe nyakati zote za maamuzi juu ya mustakabali wa maisha yako.
Hongera sana mkuu, vipi ulisota kitaa kwa muda gani hadi ukaona ni heri ujiajiri!
 
Mimi nilianza harakati za kutafuta pesa ya madafu kabla ya kuingia mtaani, nimeingia mtaani mambo hayakuniwia magumu kivilee.

Nimefanikiwa kusimamia msimamo wangu wa kutopeleka barua ya maombi ya kazi mahala popote pale tofauti na ajira ya serikali.
 
Ngoja wamalizie kuhadithiana walivyokula tunda kimasihara na mazingira gani ya hatari waliyolia tunda then watakuja.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kobelo
 
Back
Top Bottom