chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 20,834
- 26,217
Habari kutoka kwa mdau wangu wa kuaminika ambaye pia ni muajiriwa katika kitengo flani humohumo wizarani ananitanabaisha kwamba majina ya waliochaguliwa kujiunga na kada mbalimbali kupitia wizara ya afya yako mbioni kutoka muda wowote kuanzia sasa kwani zoezi limekuwa gumu sana mwaka huu kulinganisha na miaka iliyopita, kwa kifupi anasema kwa mwaka huu wizara imepokea maombi mengi sana kupita matarajio yao na uwezo wa kuwahudia wanafunzi hao,. Anasema wizara imepokea maombi ya wanafunzi takriban elfu ishirini huku uwezo wa wizara kuwahudumia wanafunzi wote hao ukiwa haupo kwani wao watahudumia wanafunzi elfu mbili tu, sasa wizara inaendelea kupitia maombi hayo huku ikiangalia wenye ufaulu wa juu,. Yaani wenye Ufaulu wa daraja A na B;.. Tuendelee kuvuta subira mpaka hapo watakapoyatoa,.