Wale wanaosubiria post za afya

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
20,834
Reaction score
26,217
Habari kutoka kwa mdau wangu wa kuaminika ambaye pia ni muajiriwa katika kitengo flani humohumo wizarani ananitanabaisha kwamba majina ya waliochaguliwa kujiunga na kada mbalimbali kupitia wizara ya afya yako mbioni kutoka muda wowote kuanzia sasa kwani zoezi limekuwa gumu sana mwaka huu kulinganisha na miaka iliyopita, kwa kifupi anasema kwa mwaka huu wizara imepokea maombi mengi sana kupita matarajio yao na uwezo wa kuwahudia wanafunzi hao,. Anasema wizara imepokea maombi ya wanafunzi takriban elfu ishirini huku uwezo wa wizara kuwahudumia wanafunzi wote hao ukiwa haupo kwani wao watahudumia wanafunzi elfu mbili tu, sasa wizara inaendelea kupitia maombi hayo huku ikiangalia wenye ufaulu wa juu,. Yaani wenye Ufaulu wa daraja A na B;.. Tuendelee kuvuta subira mpaka hapo watakapoyatoa,.
 
mkuu ujasema katika facult ipi!? na level ipi?
Manake hapa kuna cert na dip kwa hiyo funguka zaidi..
Hata hivyo tunauthamini mchango wako!
Ila funguka pamoja na source ya kueleweka mkuu!
Ili kudhihirisha we ni great thinker do more research usikurupuke aseeee!
 

hapo ndo nimefikia kikomo mkuu,.
 
maelezo niliyopewa ndiyo hayo wandugu, na hii inahusisha kozi zote,. Nyongeza ya hapo itakuwa UONGO
 
Kozi zenye competition kubwa sana ni clinical medicine na nursing. course kama pathology waombaji ni wachache
 
Kiwango cha A & B???? Technologia imewaacha nyuma sana hao wizara...toka mwez wa 4 had sasa still wanafanya selection???? This z real boring!!!!
 
Mh hao mwenye A na B wameenda advnce, wenye shida ya chuo ni wale waliopata 3 za mwisho na 4
 

Huyu amepanga awarushe roho official information ni hizi hata kuchagua bado zoezi linatarajiwa kuanza tarehe 27 sept hadi tarehe 4 oct na watakaochaguliwa kutangazwa tar 5-10/oct. Tulieni tu.
 
Huyu amepanga awarushe roho official information ni hizi hata kuchagua bado zoezi linatarajiwa kuanza tarehe 27 sept hadi tarehe 4 oct na watakaochaguliwa kutangazwa tar 5-10/oct. Tulieni tu.

We ni waziri??
 
Tumwamini nani au ndo wote tupo jela haipaswi yeyote kumuuliza mwenzie eti "Anayepita nje ni nani huyo??" Au kwa kuwa wote tupo jela harafu mmoja wetu akasikia sauti akaanza kutuambia kuwa anayekuja ni fulani, na wakati hajui lolote na sisi kumwamini ikawa tunafanya makosa, BASI TUWAACHIE WENYEWE WIZARA UKWELI NDO WANAUJUA.
 
na upande wetu tulioomba dental therapy,vipi competition yake?
 

acha kuamini kwani kuna aliyekulazimisha uamini au unataka hadi mtu ascan walaka mbona mnauliza mkijibiwa mnajifanya majibu syo yenyewe au mlishazoea mnajibiwa fyongo eti?
 
Sawa cha muhimu matokeo, na ndo yanayosubiriwa no doubt ahsanteni wote mnaotujuza kwani inaleta faraja sometimes.
 
Mnaleta masiala nyie! Which is which, usiandike kitu humu kama huna uhakika nacho.
 
sawa cha muhimu matokeo, na ndo yanayosubiriwa no doubt ahsanteni wote mnaotujuza kwani inaleta faraja sometimes.

matokeo gani kwani wewe umefanya mtihani gani hadi upewe matokeo? Halafu wewe unaonekana hata medical field huifai kwa nini usiende hata kada nyingine bwana.
Kwani majina uliyotumia kutuma maombi ni yapi?
 
matokeo gani kwani wewe umefanya mtihani gani hadi upewe matokeo? Halafu wewe unaonekana hata medical field huifai kwa nini usiende hata kada nyingine bwana.
Kwani majina uliyotumia kutuma maombi ni yapi?

Peter Emmanuel, Vipi mkuu upo kitengo nini unataka unipigie chabo??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…