Mahweso
JF-Expert Member
- Jan 10, 2014
- 1,098
- 1,501
Hebu jaribuni kuwa na fikra za utandawazi na uhuru wa kujieleza, Kama Rais wa Nchi ndugu Jakaya kikwete kila aendapo anawahamasisha Watanzania kuipiga kura ya ndio kwa Katiba pendekezwa muda ukifika na CCM katibu wao Kinana na nape hufanya hivyo? inakuwa hawa wanaoona mchakato haujaenda sawa kwa upande wao iwe kosa? ina maana CCM kila wakifanyacho ni lazima kila Mtanzania akikubali?
Waislamu kipindi cah Bunge la katiba walisema tena Bungeni, kama Mahama ya Kadhi haita wekwa kwenye katiba mpya, basi wataipigia Kura ya hapana. Na wakamwambia Waziri Mkuu asiwape ahadi ya uongo maana Serikali imewadanganya sana na Waziri Mkuu akawahakikishia.
Serikali inajua kuwa Serikali haina Dini, sasa kama wako tayari kuitengenezea Sheria hii Mahakama kwenye ngazi za Kiserikali? si nililazima kuwe na watumishi wa kuzisimamia hizo sheria? Serikali itakwepaje kugharamia hiyo Mahakama?
Ushauri wangu kwa Serikali na chama chao yaani CCM, mliwaahidi kwenye uchaguzi uliopita, sasa kama mnalazimisha iwepo ili Waislam wawachague tena mmejidanganya sana, Kama mnafikiri waislam ni wengi na ndio wenyeuwezo wa kuwaweka madarakani tena imekula kwenu. Rais Kikwete hakuchaguliwa kidini, alichaguliwa na Watanzania, sasa kama mnaleta udini mtaumia,
Kuweni makini na hilo