Wale ' Wapuuzi ' wachache wa Simba SC niliowaambieni kuwa Kocha Masoud Djuma hatufai na ' mkanidhihaki ' rudini muombe radhi

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
GENTAMYCINE sijawahi Kukosea na ukiona namsema au namchukia Mtu basi jua 99.99% ana matatizo na hafai kabisa. Asante sana Uongozi wa Simba SC kwa kuachana na Kocha ' Mnafiki ' Masoud Djuma Irambona na asanteni kwa kupanga Kumleta ' Mwanangu ' mwenyewe na Kiungo wa Ukabaji ambaye mpaka leo bado sijaona aliyemfikia Suleman Abdalla Matola a.k.a Mzambia a.k.a Veron.

Kuna ' Wapuuzi ' wachache wa Simba SC siku moja nilipoanzisha Uzi wa Kumsema na Kumnanga Kocha huyu Mburundi Djuma mlikuja Kwangu ' Kishamba ' na wala hamkunielewa kile ambacho nilikuwa nakisema na sasa yale yale mawazo yangu ndiyo yametimia na ' Mnafiki ' wenu ameshafurushwa. Na kama kuna Wana Simba SC mnajifanya mnapenda sana mnaweza mkaenda nae huko Kwao Burundi ila kwa Simba SC yetu hatumtaki.

Kocha gani kuanzia alipokuwa na Joseph Omog, akaja Pierre Lenchantre na hadi huyu wa sasa Patrick Aussems Yeye Kazi yake ni kuwapiga tu ' Majungu ' na kuwafanyia ' Fitina ' ili waonekane wabaya na hawafai ili tu Yeye akabidhiwe Timu.

Mwambieni Masoud Djuma Irambona kuwa ana ' laana ' ya hao Makocha Omog na Lenchantre na na nakumbuka kila mara Kocha Lenchantre akihojiwa kuhusu Simba SC huwa anasema hana matatizo na Klabu bali humtupia mno lawama Kocha Msaidizi Masoud Djuma na alimtabiria mwisho mbaya ndani ya Simba SC na ambao hatimaye sasa umetimia.


Nawasilisha.
 
MNAJICHEKESHAAA WENYEWEE SSC HAHAHAAA
 
Mrundi yule alikua na zengwe sana na alivyo na ngozi ya kondoo interview zako zote haachi kumtaja mungu kumbe ana husda kiasi hiki.
Mwisho wa ubaya aibu
 
Nimefatilia mpambano wa leo African Lyon vs Simba mwanzo Mwenga 😀😀😀😀😀😀😀.
 
Viongozi wa Simba wanapenda kuwa na maugomvi na makocha wazuri, timu gani haikai na kocha misimu hata miwili. Kama kocha amewapa ubingwa stick with him achana na off-pitch tantrums. Hata huyo Matola Simba walimboa akaondoka zake eti leo wanamuona lulu.
Sasa kwa style ya huyu kocha wa sasa ubingwa unaweza usipatikane, magoli machache tena ya mbinde, sub hazina macho wala masikio, refer sub za leo na African Lyon.
 

Kocha Masoud Djuma ameipa Simba SC Ubingwa lini? Kuna Watu ni ' Wapuuzi ' sijawahi kuona. Uwezo wako wa kufuatilia mpira ni mdogo sana hebu jitahidi ujifunze Kwanza kisha ukishaona umeujua karibu tena hapa Jamvini. Eti Masoud Djuma Irambona ameipa Simba SC Ubingwa. Kuna Watu mnakera humu hadi tunashindwa Kuwavumilieni. Wewe ulidhani nilipokuwa namkosoa Djuma nilikuwa napoteza tu muda wangu hapa JF? Jicho langu ni la ' dhahabu ' na likiona Kitu kiwe kibaya au kizuri jua 99.99% sijakikosea!
 
DJUMA, BORA UKWELI MCHUNGU, KULIKO UONGO MTAMU.

-Rafiki yangu Masoud Djuma amepeana mkono wa kwaheri na mabosi wa Simba. Muda wowote kutoka sasa ataenda Uwanja wa Ndege kuianza safari ya kurudi kwao Rwanda. Simba haina inachomdai na Djuma mwenyewe hana anachoidai Simba.

-Djuma anaondoka, huku nyuma akiwaacha vinywa wazi baadhi ya manazi wa Simba wanaompenda. Ameiacha sumu hii na ameipakaza sehemu kubwa. Manazi hao wanaamini kaondolewa kwa kuonewa.

-Sio kificho tena. Maneno ya Try Again jana asubuhi yamehitimisha safari ya Djuma kama kocha msaidizi wa Simba. Kama Try Again Rais wa Simba alisema wanatumia nguvu kubwa ya usuluhishi baina ya Djuma na Mbelgiji, lakini mambo yamekuwa magumu, hapa tunapaswa kutumia akili ndogo ya 2 + 2 = 4 kuelewa Djuma hana chake Msimbazi. Try Again alikuwa muwazi.

-Lakini ninachokiamini kuwa kuna siku Djuma atarudi nchi hii kufundisha soka. Kama si msimu huu, msimu ujao. Au msimu mwingine, ila atarudi. Zimwi likujualo, halikuli likakwisha. Djuma hajaondoka kama walivyoondoka makocha wengi wa Simba walioondoka hivi karibuni. Ameondoka kama dume la Nyani linalotembea kwa madaha katikati ya kundi kubwa la nyani wa kike.

-Djuma kama wanadamu wengine ana mapungufu yake. Lakini anajua kufundisha. Anajua kuifanya timu ikacheza anavyotaka. Ana identity yake ya mpira. Ni Guardiola fulani hivi wa 'bei rahisi'. Ana sex football. Anajua kumfunga mpinzani na kumtawala. Hapa ndipo Djuma alipowashika wanaompenda. Hajawashikia kwingine, ni hapa tu.

-Hawa mashabiki wa Simba waliowehuka nae sio wajinga. Kuna kitu wanakiona katika kichwa chake. Simba imewatimua Omog, Mayanja, Lechantre, sababu ni yeye, lakini hii haijafanya manazi hao waache kumuona kama Djuma mwanadamu wa ajabu, ndiyo kwanza wamemuweka vizuri katika mioyo yao na ilichokifanya Simba wanahisi kaonewa. Huu ndiyo 'uchawi' wa Djuma.

-Mashabiki hawa waliamini hata sare yao na Ndanda Fc pale Mtwara na kipigo chao cha Mbao kule Mwanza ilitokana na Djuma kutokuwepo katika benchi lao. Kuna imani fulani wameiweka kwake. Tutakapoona amerejea nchini iwe kufundisha Simba au timu nyingine tusishangae.

-Katika kipindi hiki ambacho Simba inaenda katika uchaguzi, si ajabu wagombea wakatumia jina lake kuombea kura kwa wanachama. Ni mwanachama gani asiyetaka kusikia ngoma za masikio yake likipenya neno urejeo wa Djuma kwa mara nyingine? Ni wengi, wasiomtaka ni wachache wanaohesabika kwa vidole vya miguuni, mkononi. Wengi watataka.

-Wakati mwingine inakanganya na kuleta maswali magumu unapoona Djuma huyu anayekubalika hivi, ameifanyia nini Simba? Inashangaza kidogo.bHiki kiburi chake kilipaswa kuwepo kwa Selemani Matola aliyefanyia makubwa Simba, lakini msimu wake mmoja tena kama kocha msaidizi amekuwa star. Anasifiwa kuliko inavyosifiwa Simba yenyewe.

-Narudia tena iko siku Djuma atarudi nchi hii. Naamini hivi. Siamini vingine. Ni ngumu tembo kupenya tundu la sindano, lakini ni rahisi Djuma kurudi nchini. Iwe Simba. Iwe Yanga. Kokote kule, lakini atarudi tu! Si ajabu viongozi hawa waliopeana nae mkono wa kwaheri ndiyo watakaomtumia tiketi ya ndege kumtaka arudi nchini. Hupaswi kuwaamini sana viongozi wetu wa soka. Nao wana mihemko yao.

-Tumewahi kushuhudia kwa Partick Phiri. Miaka ya hivi karibuni huyu anakuwa kocha aliyetimuliwa mara nyingi na Simba na hapo hapo kuwa kocha aliyeifundisha mara nyingi katika vipindi tofauti. Phiri anatimuliwa mchana, jioni anarejeshwa. Nasikia mwenyewe ameizoea hali hii, haimpi shida.

-Sitashituka Djuma akiwa Phiri mwingine. Kunataka moyo wa Hawafu mwenye nguvu kuachana moja kwa moja na Djuma. Djuma si Omog, Djuma si Mayanja, Djuma si Lechantre, Djuma ni Djuma tu. Yuko mmoja kama alivyo.

-Mwisho kabisa namtakia kila la kheri rafiki yangu Djuma. Safari njema my friend na fika salama, ila wacha nikunong'oneze kitu hakikisha simu yako inakuwa na chaji muda wote. Burundi na Tanzania sio mbali. Bon Voyage my friend Djuma.
 
Chunguza Watu wengi wanaomtaja sana Mwenyezi Mungu ndiyo huwa ni wabaya, wanafiki na wana roho mbaya ya Kimataifa.
Ngoja nianze kufanya uchunguzi kwenye Siasa zetu kama huu ukweli una-work
 
timu
timu yyete serious haiwezi kufanya mabadiliko ya bench lake la ufundi katikati ya ligi tena ikiwa inafanya vizuri
 
Kwani hujui kuna yule mfalme nani cijui wanamuita dikteta nae anapenda sana kumtaja mungu.... ila......


Mrundi yule alikua na zengwe sana na alivyo na ngozi ya kondoo interview zako zote haachi kumtaja mungu kumbe ana husda kiasi hiki.
Mwisho wa ubaya aibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…