Wale wazee wa vitonga tukutane hapa

Wale wazee wa vitonga tukutane hapa

Nelson Jacob Kagame

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2022
Posts
9,576
Reaction score
13,545
Kuna watu wameumbwa duniani na fani zao, leo tuzungumzie wale wazee wa vitonga.

Mjini kugumu ila ukiwa mzee wa vitonga unaona mji mwepesi maisha yanaendelea. Bali ukiwa kitonga kuna vitu lazima uwe navyo au uvifanye kwa maisha yetu ya kimjini mjini.

1: Kitonga lazima ujue kulenga eneo la tukio na aina ya watu wa kuwadandia. Sio watu wote wa kuwafanyia ukitonga

2: Kitonga lazima uwe unabadilika kutokana na mazingira, watoto wa mjini wanasema uwe na tabia ya kinyonga, usiwe na tabia moja hadi watu wakukariri.

3: Kitonga lazima ujue kucheza na akili za binadamu popote pale unapokuwa.

4: Kitonga lazima uwe na kumbukumbu sababu maisha hubadilika hivyo mbinu nazo za ukitonga lazima ziwe zinabadilika badilika.

5: Muonekano ni muhimu kwa kitonga kila unapokuwa eneo la tukio, uvae kutokana mazingira husika.

6: Kitonga lazima uwe na roho ngumu sababu ukitonga bila roho ngumu fani hii itakushinda.

7: Kitonga hana kambi, popote pale penye utelezi wa mambo unaslide hapo hapo.

8: Kitonga tanguliza mbele maslahi yako kwanza,halafu wengine ndio wafuatie.

9: Kitonga usisahau dunia uwanja wa fujo kila mbuzi atakula kwa urefu wa kamba yake sasa usikae kinyonge.

10: Kitonga uwe na fani yoyote ile iwe inakulinda dili zikiwa zimekauka.

Watu wanaidharau sana hii fani ya ukitonga ila maborn town tunajua hii ni fani kama fani nyingine na ingebidi iwe inafundishwa vyuoni kama somo la ujasiriamali.
 
Ukitonga kazi sana unaweza jifanya daktari ukamtia mgonjwa sindano la ng'ombe! Haitoshi unaweza jifanya mgonjwa ukakutana na watu waliochafukwa nyongo.

Watu waliobobea kwenye fani ya ukitonga wewe na ugonjwa wako ukalishwa vile vidonge vya kijani vya ng'ombe! Na vilivyo vikubwa vile vidonge ng'ombe mwenyewe hamezi mpk viwekwe kwenye maji ila kwa watu waliochafukwa utameza tu!
 
Ukitonga kazi sana unaweza jifanya daktari ukamtia mgonjwa sindano la ng'ombe! Haitoshi unaweza jifanya mgonjwa ukakutana na watu waliochafukwa nyongo,watu waliobobea kwenye fani ya ukitonga wewe na ugonjwa wako ukalishwa vile vidonge vya kijani vya ng'ombe! Na vilivyo vikubwa vile vidonge ng'ombe mwenyewe hamezi mpk viwekwe kwenye maji ila kwa watu waliochafukwa utameza tu..!
Daaah mkuu umenichekesha😂🤣🤣🤣🤣Unafanya ukitonga hospitali kufuata mchongo,kumbe na daktari unaekutana nae nae kitonga yupo pale kimkakati🤣🤣🤣🤣🤣.Risk zipo tu kwenye fani yoyote mkuu
 
Daaah mkuu umenichekesha😂🤣🤣🤣🤣Unafanya ukitonga hospitali kufuata mchongo,kumbe na daktari unaekutana nae nae kitonga yupo pale kimkakati🤣🤣🤣🤣🤣.Risk zipo tu kwenye fani yoyote mkuu
Unaweza jifanya mchungaji ule pesa za waumini kumbe waumini nao wapenda vitonga! Mbaya sana kuwachanganya malaika wa Mungu na shetani mnaweza kupigwa mapigo pande zote mbili!

Ushawahi kutenda dhambi mpaka shetani anatoa note book ananakili dhambi yako? Sasa jiulize kwanini ainakili? Kuna dhambi hajawahi kuziona.😅
 
Kitonga usijinunulie bia peke yako kama mko wa3 mezani, zungusha round mzee uwashtue wana halafu subiri mserereko
 
Unaweza jifanya mchungaji ule pesa za waumini kumbe waumini nao wapenda vitonga! Mbaya sana kuwachanganya malaika wa Mungu na shetani mnaweza kupigwa mapigo pande zote mbili! Ushawahi kutenda dhambi mpaka shetani anatoa note book ananakili dhambi yako? Sasa jiulize kwanini ainakili?
kuna dhambi hajawahi kuziona..😅
Mwanangu mmoja anaitwa Isaack,kanichukua toka home enzi hizo nipo dogo nimemaliza form four.Tukaenda kariakoo kuna sehemu wanauza computers used,mimi sijui kumbe bro kampiga mchungaji wa mchongo wa kipentekoste computer kumi desktop na alizileta pale kuziuza.

sasa siku hiyo nilimsindikiza akachukue hela yake kumbe mchungaji kashapata fununu yupo pale na wapambe kibao wanatusubiria watudake.

Bro machale yakamcheza kumuona mchungaji na wapambe zake akajifanya anaenda chooni akasepa,mwenye ofisi nae machale yakamcheza kuona kumuona mchungaji na wapambe wake akasepa akamuacha msaidizi wake na mimi pale dukani.

Kumbe mchungaji nae zile computer desktop kazipiga sehemu kuna watu wana rb yake🤣🤣🤣🤣 na wapo na polisi wanasubiria wamdake.Ilikua noma maana na mimi nikajifanya mteja sijui chochote sikuja na brother🤣🤣😂😂.
 
Kuna watu wameumbwa duniani na fani zao,leo tuzungumzie wale wazee wa vitonga.Mjini kugumu ila ukiwa mzee wa vitonga unaona mji mwepesi maisha yanaendelea.Bali ukiwa kitonga kuna vitu lazima uwe navyo au uvifanye kwa maisha yetu ya kimjini mjini...
Kwa hiyo unakuwa mwanaume halafu unakuwa unapiga mizinga hovyo na kudandia pombe za bure za wanaume wenzako?

Hapo kifiro kinakuhusu
 
Asalaleeee...😂
Mkuu zilipigwa ngumi hapo🤣🤣🤣😂Afu kariakoo hakuna dogo watu kibao,mchungaji wa mchongo full kuvuja damu,pale dukani baadhi ya vitu viliibiwa.Wakazibeba zile computer wakaenda kituoni kumalizana maana ilibidi mwenye duka arudi kutuliza msala ila bro mda huo huo keshapanda abood kukimbilia mji kasoro bahari kusikilizia kwanza.🤣🤣😂😂
 
Kwa hiyo unakuwa mwanaume halafu unakuwa unapiga mizinga hovyo na kudandia pombe za bure za wanaume wenzako?
Hapo kifiro kinakuhusu
Hii fani msomi,vitonga wanaishi poa sana hapa town. Afu vitonga professional sio walevi bali wanaslide na ukitonfa kwenye michongo ya maana sio ofa za pombe au mademu.
 
Hata wewe mtoa mada ni mzee wa kamseleleko. Unajisaulisha eeeh😎
 
Kuna watu wameumbwa duniani na fani zao,leo tuzungumzie wale wazee wa vitonga.Mjini kugumu ila ukiwa mzee wa vitonga unaona mji mwepesi maisha yanaendelea.Bali ukiwa kitonga kuna vitu lazima uwe navyo au uvifanye kwa maisha yetu ya kimjini mjini.
town tunajua hii ni fani kama fani nyingine na ingebidi iwe inafundishwa vyuoni kama somo la ujasiriamali.
Kwa mazingira haya ya ukosefu wa ajira napendekeza iwe ni somo kwenye ujasiriamali😂.Japo tugawane umaskini kwa hiari🏃
 
Hii ni zaidi ya "Bongo Dar es salaam" ya Prof. J
Mzee ilikua noma afu bro kanikimbia sina nauli,ilibidi nipige mdogo mdogo kutoka kariakoo mpaka kinondoni mkwajuni🤣🤣🤣🤣 kwa bi mkubwa wake kumpa habari za mwanae
 
Je hawa wazee wa vitonga, wana tofauti gani na hawa 'CHAWA' , 'CHAWA Pro', 'CHAWA Pro Max'
Chawa watoto wa juzi.Vitonga wamekuepo toka enzi za julius🤣🤣🤣.Toka enzi za Kabanga Mwitambe professa katika ukitonga
 
Back
Top Bottom