Wale wote wanaotumia bidhaa za kampuni ya Xiaomi tukutane hapa ili kupeana ujanja

Wakuu sangawejr, deojames kwahiyo issue ya simu yangu nisahau maana sijapata msaada effectively
Mkuu hata mimi sina solution kwasasa
Kama una contact na aliekuwa owner akusaidie itakuwa safe zaidi kuliko hizi njia zingine za ku flash nk.
 
Karibu kwenye ulimwengu huu mkuu...
 
Hizo Earphone umechukua kwa Sh ngapi??
 
Hayawi hayawi hatimae yamekua nw, tunasubiri leo update ya miui 11 kama walivyoahidi, kwani ni leo hii Mwenye uelewa zaidi au info zaidi atuwekee hapa
 
Hayawi hayawi hatimae yamekua nw, tunasubiri leo update ya miui 11 kama walivyoahidi, kwani ni leo hii Mwenye uelewa zaidi au info zaidi atuwekee hapa
Sisi wenye Note 6pro, ngoja tukae kimya maana hatukupewa priority kwenye hiyo update.
 

Cheki live stream yao bado wanapresent Miui 11 naona nzuri. Nitawapa info zaidi ikiisha
Hayawi hayawi hatimae yamekua nw, tunasubiri leo update ya miui 11 kama walivyoahidi, kwani ni leo hii Mwenye uelewa zaidi au info zaidi atuwekee hapa
 
MIUI 11 kwenye presentation nimeona vitu hivi: Design mpya, Fonts mpya, sounds mpya, Always on Display themes mpya, Mi work ( file manager, screen cast, print), Mi go (itakusaidia kwenye kupanga safari) na super battery saver

Beta inaanza 27 September.

Release wamesema ni mid October kwa kila device.

Watu wenye mi account wanaweza kujaribu leo kuanzia usiku.

Though itakuwa Chinese version, information kuhusiana na global rom wamesema watatoa baadae
 

Yeah ndio wana release leo imeanza kwenye hii simu mpya Mix Alpha, ila mchina anajua sana.
 
Nina mzigo umekwama sehemu moja siku 18. Tracking inasema Arrival at Destination Post (Country: TZ).
Nikitrack kwenye website ya Posta inasema No information available for this shipment
Nini cha kufanya wadau
 
Siyo mimi niliyonunua..muda umepita tangu uulize ilo swali na hujajibiwa, scan ujue
Basi mkuu sio kesi NGOJA NIMSUBIRI KAZETELA alete jibu/link [emoji16]
Ukiscan kwa picha zinakuja picha za bidhaa kama 1000 hivi za Earphones hizo ,ntajua ipi ni ipi?,unajua mpaka amenunua/kununuliwa ina maana bidhaa aliichunguza kwa makini.

Humu huwa tunasaidiana kwa kumpa mtu LINK ya Bidhaa husika ndio rahisi zaidi na sio KUSCAN
Anyway Mchana mwema
 
Mkuu hizo earphone mdau post za nyuma alisema anajaribu kuagiza bidhaa ya bei ndogo aone kama mzigo utamfikia. Ndio akaagiza hizo earphone. so hapo bei ni kuanzia 2000 hadi 10,000.
Hivyo yawezekana hakuzingatia ubora nk.

Na ukumbuke hizo ni copy za product ya Apple.
 
Huu mzigo mkuu nenda posta utapata majibu vizuri. Yawezekana upo tu posta huo mzigo hata kama upo mkoani kwa huo muda hapo yawezekana mzigo ulishafika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…