Wale wote wanaotumia bidhaa za kampuni ya Xiaomi tukutane hapa ili kupeana ujanja

Jema mfano Seller kaandika 45$ ila wakaja TRA wakasema hii sio bei halisi wakati seller kaandika hiyo hapo inakuaje?
 
Jema mfano Seller kaandika 45$ ila wakaja TRA wakasema hii sio bei halisi wakati seller kaandika hiyo hapo inakuaje?
Jamaa wanakuwaga na mikwara mbuzi so wanakujambisha uwape bei halisi, mkibishana sana unachomoa invoice yako (printable) na kuwapa ili kuongeza Uzito maana hiyo ni document inayokubalika na kila kitu kipo wazi kwenye andiko plus muhuri na namba za mawasiliano ikibidi wa Mpigie tu seller awape uthibitisho.
 
Anhaa hapo sawa
 
Anhaa hapo sawa
Tunapo kwama ni kukosa hiyo invoice maana jamaa wa TRA wakiuliza bei ukawatajia dolar 50 nao wakabisha kwamba hiyo bei siyo halisi mtabishana na watataka uwaonyeshe uliponunulia wathibithishe!!!
Nawe huna chochote Cha kuthibitisha so yabidi uufyate tu kwao maana wakikadiria kivyako utaumia mkuu.
 
Jema mfano Seller kaandika 45$ ila wakaja TRA wakasema hii sio bei halisi wakati seller kaandika hiyo hapo inakuaje?
Why Hao jamaa wapingane na Invoice toka kwa suppliers?
Kwavile ni 45$?
Kama watatakuwa wanakadiria kwa kufananisha na Tecno f'lani hivi watakuwa wanafeli!!!
Mbona Kuna madude huko yanauzwa chini ya 40$ mfano hilo la chini hapo.


 
Mi waliniambia niwafungulie page ya seller AliExpress wahakiki Bei niliyonunua kijana mweupe yule anajifanya anakamia sana
Hukuwa na invoice au kithibithisho chochote cha bei nao walitaka wajiridhishe afu huwa wanakaba makusudi wakijua kwamba huwezi kuiacha simu yako kali.
mimi nina kawaida ya kufungulia parcel pale kidirishani ili kuhakiki kama kila kitu kipo sawa sasa kuna siku niliitoa Redmi note 7 kwenye zile Buble si yule mama akaning'ang'ania niivue kwa box ili aione live maana kaipenda ile picha juu ya box nikamwambia kifaa cha watu hiki siwezi kuondoa seal bila ya ridhaa ya mwenyewe.
Kuuliza bei nikamwambia mia na 20 akaiponda kumbe ndogo kuliko spark 7 yake nikamwambia poa haina shida.
mida mida huwa tunajirengesha wenyewe kwa hawa watu so tuwe makini katika kujibu maswali yao.
 
Hapo nimekupata mkuu umenipa elimu nzuri
 
Bahati mbaya hakuniuliza
alichoanza ni kuniambia nimuoneshe Bei kwenye page ya AliExpress ajue Bei halisi ya mzigo, wala hakuniuliza Bei ya mzigo
 
Wakuu Bajet ya 380K mpaka 400K
Naweza Pata xiaomi ya aina gani maana mmenivutia nihamie kwenye hii familia

Naombeni mwongozo tafadhali
Anza na huyu mnyama ndo natumia hata mimi muda huu, iko vizuri ila sijajua ww kipaumbele chako kwenye simu nini
 
Mkuu hyo simu inafanya kazi bongo kweli, nazionaga simu bei ya chini alliexpress Ila sababu hazna majina naogopa tcra wasije kua wamezifungia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…