Walevi wa Madaraka wanapanga safu, wanaisigina ilani

Walevi wa Madaraka wanapanga safu, wanaisigina ilani

Joined
Jul 6, 2024
Posts
97
Reaction score
72
Wakubwa baadhi wenye vyeo Walevi wa Madaraka Wabinafsi wanapanga safu. Wanatutemea mate kwa kusigina ilani, katiba, kanuni, miongozo na taratibu za Chama. Wanaweka viongozi walio kinyume na matakwa ya maandiko ya kimfumo.

Wanatumia michawa mijinga jinga kusifu uovu ambao utawanufaisha hao baadhi ya viongozi waovu. Na michawa kwa ukosefu wa uzalendo inacheka cheka kama mizuzu na kuwashangilia waovu kwa malipo ya kununuliwa ubwabwa.

Huu sio uzalendo. Uzalendo ni kuwa tayari kuufia ukweli. Nasema, mkubwa akijaribu kunitemea mate huku nikiwa njia sahihi, mimi nitamtemea kohozo zito lenye vidudu vya TB.

Tumechoka kunyenyekea ujinga na upumbavu. Nimemuelewa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kupitia clip hii. Siko tayari kurudi nyuma.

Tusome katiba ya CCM 1977 toleo 2022 ibara 05(04). Kanuni za uongozi na maadili za CCM na jumuiya zake toleo 2022 uk 02 ibara 04 kwa msisitizo. Ilani ya CCM 2020 uk 01 ibara 04. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 toleo 2005 ibara 26(1)(2), ibara 09a, b, f, na h.
 
Back
Top Bottom