Wali moto, mchuzi moto

kakuruvi

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2009
Posts
770
Reaction score
258
Salam JF's woote,

Valentine ndiyo hiyoo, tusubiri ya mwaka ujao panapomajaliwa, mwenzetu mmoja alipata msukosuko ila aliumaliza kiutu uzima.
Jamaa walikorofishana na mama watoto wake mpaka ikafikia mamaa kufungasha nguo zake ili asubuhi aondoke, usiku jamaa akamuuliza vipi mbona unafungasha? mkewe akajibu asubuhi naenda kwa mama yangu, jamaa hakupata usingizi, asubuhi akawahi kuamka mapema akaanza na yeye kufungasha mkewe akamuuliza mbona unafungasha? jamaa akamjibu naenda kwa mama yangu, mkewe kwa mshangao akamuuliza tena unaenda kwa mama yako watoto je? Jamaa akamjibu wataenda kwa mama yao..
Zoezi la kwenda kwa mama liliishia hapo na wote wakaelekea kazini. Wana JF nani mjanja hapo?
 
Mi hapo naona watoto ndio wajanja,
maana kila mtu ni mtoto kwaw mama yake
 
Hiyo kali kwa kweli, namsifu jamaa alikuwa na strategy nzuri.
 


Duh!! this is just too good! imenifurahisha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…