Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
WALI WA ASUMINI
Mchele kilo 1
Kuku mkubwa 1
Vitunguu maji kilo 2
Mayai 8
Samli kilo 1
Thomu gram 200
Tangawizi mbichi gram 50
Mdalasini gram 50
Hiliki gram 50
Bizari nzima kiasi
Siki kiasi
Mtindi painti 1
Tungule kilo 1
Zabibu nyeusi kiasi
1 Mkate kuku umwoshe umchemshe kwa maji na chumvi mpaka awive, kisha muepue.
2 Menya vitunguu uvioshe uvikate na uvigawe sehemu mbili. Sehemu moja uiweke, sehemu ya pili vikaange mpaka viwe vyekundu kama vya biriani. Kisha
vichuje uitoe samli yote, vitie katika sinia uvitandaze ili vipoe kwa kupata upepo.
3 Chukua mdalasini, hiliki na bizari utwange pamoja, kisha uchunge unga laini. Saga thomu na tangawizi mbichi. Saga tungule.
4 Teleka sufuria tia samli ile ile iliyokaangiwa vitunguu halafu utie vile vitunguu vilivyobakia uvikaange. Vikianza kuiva tia viungo ulivyovitwanga na
kuvisaga. (Bakisha vitunguu na viungo kidogo). Tia vipande vya kuku, mtindi siki na supu ya kuku iliyobakia katika sufuria. Acha ichemke nyama pamoja na
vitu vyote mpaka libaki rojorojo.
5 Teleka maji, yakichemka tia chele. Ukiiva utoe uchuje yatoke maji yote.
6 Teleka tena sufuria utie samli kidogo utie na vile vitunguu ulivyovibakisha uvikaange. Tia mdalasini nzima, kaanga pamoja, tia na ule wali ukoroge
koroge ili uchanganyike na viungo. Kisha ufunike upalie moto.
7 Chemsha mayai yote uyamenye.
8 Wali ukishakauka utaupakua, lakini lazima itabidi utumie kombe au sahani kubwa itakayoweza kuingia wali pamoja na vitu vyote. Kuupakua kwake
kwanza utatia nusu ya wali katika hiyo sahani, baadae utatia masalo na nyama yote, na mayai, kisha utayafunika masalo kwa wali uliobakia. Mwisho
utachukua vile vitunguu ulivyovikaanga na ukavitandaza ili vipo, utavimwaga juu ya wali.Kwani ni kwa sababu ya hivi vitunguu ndio maana ukaitwa wali wa
asumini. Ukipenda utapamba chembe za zabibu juu yake. ZABIBU HIZO Ziroweke kwanza ili zivimbe.