Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Mchele wa brauni,unaojulikana zaidi kwa jina la kiingereza Brown rice,Ni mchele wenye wanga salama na unabeba virutubisho vingi kuliko mchele mweupe ,vitamin B1,B3,fatty acids,magnesium,iron na nyuzi nyuzi zifaazo katika usagaji wa chakula mwilini

Mchele huu ni mzuri sana kwa afya na unafaa sana kwa wagonjwa wa kisukari,moyo na watu wanaojali afya zao kwa kuzingatia virutubishoo wanavyoingiza mwilini.
Unapokua kwenye dayati wali huu unafaa sana,hivi ndivyo nilivyoupika juzi
Mahitaji
Njia
Kama maandalizi ya awali loweka mchele kwenye maji ili uloane,mchele huu ni mgumu sana kuiva hivyo ni vyema kuuloweka kwa muda ili ulainike.
1.Katika sufuria weka mafuta,vitungu maji,binzari zote,na vitunguu saumu.kaanga kwa pamoja kwa moto mdogo adi vitunguu maji visinyae kabisa ila visibadilike rangi kua brauni
2.Ongeza nyanya ya kopo,chumvi na giligiliani,changanya kisha ongeza maji robo kikombe ili kuivisha viungo,pika adi maji yaelekee kukauka.
3.Ongeza mchele kisha kaanga kwa muda ili viungo vishikane na mchele.ongeza maji mengi kiasi,funika,ivisha wali.wali ukielekea kukauka,ongeza karoti na ugeuze wali. kisha banika ukiwa bado na maji kidogo.ni vyema ukaufunika na foili ili kutunza joto ambalo litasaidi kuivisha wali.Banika kwa muda adi wali uwe laini kabisa kama wali mweupe wakawaida.
Adi hapo wali tayari kabisa kwa kula.unaweza kula wali huu na mboga yoyote upendayo.Mimi nilikula wali huu na curry ya koliflawa pamoja na kachumbari kama ionekanavyo kwenye picha.

- Mchele wa brauni vikombe 2 (brown rice)
- Mafuta kijiko kimoja cha chai (tumia mafuta yatokanayo na mbegu za mimea)
- Vitunguu maji 4
- Vitunguu saumu robo kijiko cha chai
- Binzari nyembamba robo kijiko cha chai
- Binzari manjano robo kijiko cha chai
- Nyanya ya kopo kijiko 1 cha chai
- Giligiliani ½ kijiko cha chai
- Karoti nusu kikombe (kata boksi)
- Chumvi kwa ladha upendao
- Maji