NZURI PESA
JF-Expert Member
- Mar 25, 2011
- 5,958
- 2,954
Mapishi ya wali wa nazi:
VIFAA
Mchele kg 1
Nazi 2 au pkt 2 nazi ya maji
Chumvi kijiko 1 cha chakula
Jira kijiko 1cha chakula
Maji 1/2 lita
JINSI YA KUANDAA
Osha mchele vizuri,chuja mchanga.
Bandika sufuri yenye nusu lt ya maji safi yakipata moto weka nazi yako jira na chumvi kisha koroga hadi yachemke.Kisha tumbukiza mchele wako funika hakikisha moto si mkali sana.Subiri kwa dakika 20 wali wako utakuwa tayari. waweza kula kwa mboga yoyote.
jeko la oryxgasmkuu sawa hiyo dakika 20 ni kwa jeko lipi la gesi au mchina maana langu ni la china
jeko la oryxgas
Upate na ule ukoko wake. Bila hata mchuzi unaendaNaupenda wali wa Nazi hatari..
Angel Nylon.Upate na ule ukoko wake. Bila hata mchuzi unaenda
jeko la oryxgas
Wali mtamu ni ule uliopikwa na jiko la mkaa.
Wali mtamu ni ule uliopikwa na jiko la mkaa.
Tena sie wa pwani hayo matandu tunayaita MAHABA na hayo huwa anaekewa "MZEE"!
jira ni jira 😩