Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
WALIFIKAJE TAREHE 7 JULAI 1954 NA KUUNDA TANU NA TUNAWAADHIMISHAJE WAZALENDO HAWA?
Kuna mtaa Dar es Salaam sisi tulimezaliwa tumeukuta ukiitwa Stanley Street.
Baada ya kupatikana uhuru mtaa huu ukabadilishwa jina ukaitwa Aggrey Street kisha baadae wakati marehemu Kitwana Kondo alipokuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam ukabadilishwa tena jina ukaitwa Mtaa wa Max Mbwana.
Mtaa huu umepewa majina ya watu maarufu watatu ambao wote wamekuwa na uhusiano wa kihistoria kuanzia Tanganyika hadi kufika Tanzania.
Henry Morton Stanley ndiye aliyetumwa kuja Tanganyika kumtafuta David Livingstone na akamkuta Ujiji. Dr. Aggrey alikuwa Mwafrika kutoka Ghana.
Umaarufu wake unatokana na kuwa yeye alikuja Tanganyika mwaka wa 1924 akiwa mmoja wa wajumbe wa kamisheni iliyokuja Tanganyika kuja kuchunguza elimu ya Waafrika.
Wajumbe wengine wote waliobakia katika kamisheni hii walikuwa Wazungu.
Kleist Sykes anaeleza katika mswada wa maisha yake alioandika kabala ya kifo chake mwaka wa 1949 kuwa alikuwa Dr. Aggrey ndiye aliyemtia hima aunde African Association.
Dr. Aggrey alimpa Kleist ushauri huu baada ya kutambua kuwa Waafrika wa Tanganyika hawakuwa na umoja wao, wakati Wazungu, Waasia na Waarabu wote tayari walikuwa na jumuia zao.
Katika mswada wake ule Kleist anasema kuwa Waafrika waliwakiishwa na Father Gibbons kutoka Misheni ya Minaki ambae yeye anastaajabu kwa kuwa hakuwa na uhusiano wala muiingiliano wowote na Waafrika wa Tanganyika.
Father Gibbons ni huyo wa kwanza waliosimama kushoto kwenye picha.
Kwa sifa hii ya Aggrey kuja Tanganyika akiwa Mwafrika msomi Jiji la Dar es Salaam wakabadili jina la Stanley na kuliweka jina la Dr. Aggrey.
Kitwana Kondo akiwa Meya wa Dar es Salaam akabadili tena jina la mtaa kutoka Aggrey ukaitwa Mtaa wa Max Mbwana.
Mzee Max Mbwana alikuwa mmoja wa wazee maarufu wa Dar es Salaam waliounga mkono harakati za kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.
Baraza la Wazee wa TANU 1955 katika picha hapo chini:
1. Abdallah Shomari (Tandamti Street No. 3)
2. Nassoro Kalumbanya (Simba str.)
3. Said Chamwenyewe (Aggrey/Congo Street)
4. Mtoro Ally (Muhonda Street.)
5. John Rupia (Misheni Kota)
6. Julius Nyerere( Pugu Sekondari)
7. Said Chaurembo (Congo/Mkunguni Street.)
8. Jumbe Tambaza( Upanga)
9. Sheikh Suleiman Takadir (Mafia /Swahili)
10. Dossa Aziz ( Mbaruku /Somali Kipande Street )
11. Mshume Kiyate (Tandamti Street)
12. Juma Sultan (Kitchwele karibu na kanisa dogo )
13. Maalim Shubeti (Masasi/Likoma Street)
14. Rajab Simba (Kiungani Street)
15. Waziri Mtonga (Kilosa no. 18, Ilala)
16. Mwinjuma Mwinyikambi (Mwananyamala)
17. Maxi Mbwana ( Aggrey /Kongo Street)
18. Usia Omari (Sungwi ,Kisarawe)
19. Sheikh Issa Nasir (Bagamoyo)
Kulia wa pili waliokaa Sheikh Suleilan Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU 1954 - 1958) (Swahili/Kariakoo Street)
Muhimu kufahamika ni kuwa Jiji la Dar es Salaam lilipotoa jina la mtaa wa huu kwa Dr. Aggrey hawakutoa kwa kuenzi ile fikra yake ya kuwataka Waafrika waunde African Association.
La hasha, jina la mtaa lilitolewa kwa ile sifa yake ya yeye kuwa Mwafrika msomi aliyefika Tanganyika wakati ule wa ukoloni.
Max Mbwana alipewa mtaa kwa mchango wake katika kuunga mkono TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.
Historia ya TANU inaanza hapa alipofika Dr. Aggrey Tanganyika na kumshauri Kleist na wenzake kuanzisha umoja wa Waafrika wa Tanganyika.
Hata hivyo ilimchukua Kleist miaka mitano hadi 1929 kuasisi African Association akiwa katibu muasisi na rais muasisi akiwa Cecil Matola.
Mkutano wa kuunda African Association ulifanyika nyumbani kwa Cecil Matola Mtaa wa Ndanda na Masasi.
Nyumba hii baadae ikaja kununuliwa na John Rupia na ipo hadi leo.
Waliokusanyika pale kuasisi African Association walikuwa Kleist Sykes, Cecil Matola, Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamis, Zibe Kidasi, Ali Said Mpima, Suleiman Majisu, Raikes Kusi na Rawson Watts.
Hili lilikuwa kundi la wazalendo tisa walioanza kufunga safari ngumu ya kuelekea New Street kuja kuunda TANU tarehe 7 Julai 1954.
Bahati mbaya sana ni kuwa wazalendo hawa hawafahamiki katika historia ya Tanganyika na kwa hakika historia hii isingelijulikana kama Kleist asingeandika historia ya maisha yake.
Mswada wake huu ulichukua miaka 24 hadi 1973 kufikia kuchapwa na kama si juhudi za John Iliffe mswada ungebaki kama ulivyoandikwa na mwishowe kutoweka kama zilivyotoweka nyaraka nyingi katika historia ya Waafrika wa Tanganyika.
Mswada huu ulichapwa katika kitabu alichohariri Iliffe, ‘’Modern Tanzanians,’’ kilichopigwa chapa na Tanzania Publishing House.
Nyaraka hizi za Sykes zimesaidia sana katika kuhifadhi si historia hii ya African Association bali hata historia ya TANU.
Abdul Sykes alimpa mswada huu pamoja na nyaraka nyingine binti yake Daisy, wakati ule mwanafunzi Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na kupitia nyaraka hizi mwalimu wake wa historia, John Ilife aliweza kujua mengi ambayo yalimsaidia katika kuiandika kwa uhakika historia ya African Association.
Nyaraka hizi ndizo nyaraka pekee zilizoweza kuhifadhiwa kutoka kwa waasisi wa African Association waliokuwapo kati ya mwaka wa 1929 hadi 1954 ilipokuja kuasisiwa TANU.
Kushoto katika picha hapo chini: Mwinjuma Mwinyikambi, Max Mbwana Julius Nyerere na Mshume Kiyate, 1962.

Ufunguzi wa ofisi ya African Association New Street akiwapo Gavana Donald Cameron wa nne kushoto mstari wa kati, mstari wa nyuma kutoka kushoto wa sita ni Kleist Sykes, mstari wa mbele suti nyeusi ni Mwalimu Mdachi Shariff na mbele waliokaa kitako wa pili kushoto ni Ramadhani Mashado Plantan 1933.