Elections 2010 Waliitwa wapiganaji ndani ya CCM, mbona hawako vitani Igunga?

wapiganaji hao mahiri hawajaenda igunga manake modality ya vita imebadilika. hii ya sasa ni biological war,wameenda lab technicians manake chama hakijajiandaa so hakuna biotechnologists wa kutosha.
 
wanasiasa kigeugeu! watz kigeugeu, raisi wetu kigeu kigeu, mafisadi nao vigeugeu, dr. slaa sometimes nae kigeugeu!...mashehe wa bakwata vigeugeu, maaskofu vigeugeu......aaaaaagh!!!
 
CCM ina jeshi kubwa, kwa nn watumie bunduki kumuua nzi ? walio enda igunga wanatosha kuwapakata CDM na kuwafanya watakavyo

Sisi tuanjua CCM iko kwenye makundi makuu mawili, mafisadi na wale wanaojipambanua ni makamanda wa kupambana na ufisadi, japo hata hawa ni undumila kuwili ndio unaowasumbua.

Hii ndiyo nafasi pekee ambayo CCM ilitakiwa kujisafisha mbele ya jamii, ingeendelea na hoja hiyo hiyo ya kujivua gamba hata Igunga bila kujali ushindi. Hata kama wangepoteza jimbo la Igunga, hiyo ingekuwa ni gharama ndogo sana ya kulipa katika kurudisha imani kwa wananchi.

Mfano mdogo ni CDM arusha, wamewatimua madiwani licha ya kujua kuwa yawezekana wasishinde uchaguzi mpya utakapoitishwa. Lakini hii ni gharama ndogo sana ukilinganisha na faida ya kutokucompromise principle na misimamo ya chama.
 
Subiri uchaguzi wa Igunga upite keshokutwa, kama ccm hawatachukua ubunge, hawa wanaoitwa wapiganaji wa ufisadi na kuvua magamba lazima yawarudi wao na mtashuhudia wakivuliwa gamba wao la sivyo hamtasikia tena stori za gamba tena
 
Twaweza kusema hawajui ni nini watakachoongea igunga au ndo tuseme inakua kibalua kikali kwao je wakati wa kampeni waseme yakwamba mgombea wao ataendeleza yale mema aloyaanzisha Rostam wakati mema yenyewe hayapo kama wanafiki wengine wanavyowadanganya wana igunga
 
Samahani mtoa mada hapa jf hamna wakereketwa ila kuna great thinkers hao wakereketwa wako ccm
 
akihutubia mkutano wa hadhara.
Hapana hakuwa anahutubia mkutano wa hadhara hapa alikwenda kuwapa pole watoto kwa kufiwa na mtoto mwenzao kwa kugongwa na gari ya Magamba kabla Rostam kumstukia kwamba kaingia kinyemela na kumtimua na kupiga marufuku asionekane tena Igunga
 
Kwa hili nawatetea Magamba kwamba wao wanavikosi viwili, Mafisadi na Wanaojiita wapambanaji. Kwanza wanajaribu kikosi chao wanachokiamini kwamba kinajua mbinu zote za Uchakachuzi na wakishindwa hapa huenda next election watajaribu hicho kikosi cha pili kujaribu bahati yao. Na huu ndio utakuwa mwisho wao baada ya kujaribu vikosi vyao vyote na kushindwa na CDM chama Dume
 
Wataendaje igunga wakati tayari mahakama kuu imeridia malipo ya dowans, kwa hiyo wataumbuka
 

Penye RED FONT pamekaa vizuri.
Aksante
 
Nepi hawezi kwenda kwenye siasa uchwara , ataambulia zaidi watoto na wakina mama wazee ambao bado wanajua Nyerere bado yupo Hai
 
Nepi hawezi kwenda kwenye siasa uchwara , ataambulia zaidi watoto na wakina mama wazee ambao bado wanajua Nyerere bado yupo Hai, alafu suala la siku tisini za kuvua magamba zimekwisha kwa gamba moja tu mengine yamekakamaa na yamekomaa kuyavua labda uondoke na ngozi ngozi yenyewe ndio CCM.
 
Kinachinishangaza hao kina Mkapa na Mangula siwasikii kabisa , kulikoni?
 
Kwa kifupi CCM ina hard time. Ngoja tuone nini kitafuata baada ya uchaguzi wa Igunga.
 
Anataka kufungua shule au ndiyo kufunika kunakoitwa na CCM, hahahahaha na baaada wataanza kutafuta vichanga hospitali badala ya hawa wanafunzi!!
 
akihutubia mkutano wa hadhara.

Wakuu hapa siyo IGUnga jana? Macho ya uzee haya sioni vizuri - ha ha ha

Naona mkuu wa uenezi sasa anakijenga chama maana anahutubia vi-chipkizi vya CCM ijayo.
 
Ukijiunga na ccm uwezo wa kufikiri na kuchukua maamuzi unapungua. Hii ni ishara tosha kuwa RA ni zaidi ya tumjuavyo ndani ya ccm.
 
Haya mambo yanachanganya sana. Bashe amewahi kunukuliwa akisema anataka ccm washindwe Igunga ili waheshimiane. Wakati hawa wanaojiita makamanda wakizuiliwa kufika Igunga, Bashe huyohuyo kaenda kutafuta muafaka na cdm, sijui alitumwa na chama chake au tajiri yake Rostam. Siasa za Tanzania ni burudani, tusubiri tuone mshindi atakuwa nani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…