Walikuja walokole kutaka kuniombea eti niwe tajiri

Malaria 2

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2023
Posts
6,846
Reaction score
10,288
Jana wakati nipo nimekaa wakaja walokole 5 na mgeni 1.
Wakaniuliza nina matatizo gani? Yaani changamoto gani ktk maisha inanisumbua.
Nikawaambia sina pesa . Jamaa wakaniambia nifumbe macho tuanze kuomba kwa jina la Yesu nitakuwa tajiri.
Nikiwatizama wenyewe wamevaa yebo yebu , mguu kuku mguu bata.
Nikacheka sana. Nikawa najiuliza kimono kimoyo wao hawataki kuwa matajiri mbona wenyewe wamechoka?
Nikawaambia basi , nikasema kimoyo kimoyo wasije kunitupia mapepo
 
Sasa kama kuna kitu kibaya kinazuia usiwe tajiri kwa nini usiombewe pepo hilo likutoke? Wamefanya vema watu hao unaowaita kwa kejeli eti ni walokole
 
Jana wakati nipo nimekaa wakaja walokole 5 na mgeni 1.
Wakaniuliza nina matatizo gani? Yaani changamoto gani ktk maisha inanisumbua.
Nikawaambia sina pesa . Jamaa wakaniambia nifumbe macho tuanze kuomba kwa jina la Yesu nitakuwa tajiri.
Nikiwatizama wenyewe wamevaa yebo yebu , mguu kuku mguu bata.
Nikacheka sana. Nikawa najiuliza kimono kimoyo wao hawataki kuwa matajiri mbona wenyewe wamechoka?
Nikawaambia basi , nikasema kimoyo kimoyo wasije kunitupia mapepo
Ulivyowatazama, wao wenyewe wana dalili za kuwa matajiri?
 
Jana wakati nipo nimekaa wakaja walokole 5 na mgeni 1.
Wakaniuliza nina matatizo gani? Yaani changamoto gani ktk maisha inanisumbua.
Nikawaambia sina pesa . Jamaa wakaniambia nifumbe macho tuanze kuomba kwa jina la Yesu nitakuwa tajiri.
Nikiwatizama wenyewe wamevaa yebo yebu , mguu kuku mguu bata.
Nikacheka sana. Nikawa najiuliza kimono kimoyo wao hawataki kuwa matajiri mbona wenyewe wamechoka?
Nikawaambia basi , nikasema kimoyo kimoyo wasije kunitupia mapepo
Mbona hukuwauliza miongoni mwao walikuwepo matajiri wangapi?
 
Jana wakati nipo nimekaa wakaja walokole 5 na mgeni 1.
Wakaniuliza nina matatizo gani? Yaani changamoto gani ktk maisha inanisumbua.
Nikawaambia sina pesa . Jamaa wakaniambia nifumbe macho tuanze kuomba kwa jina la Yesu nitakuwa tajiri.
Nikiwatizama wenyewe wamevaa yebo yebu , mguu kuku mguu bata.
Nikacheka sana. Nikawa najiuliza kimono kimoyo wao hawataki kuwa matajiri mbona wenyewe wamechoka?
Nikawaambia basi , nikasema kimoyo kimoyo wasije kunitupia mapepo
Wakuombee uwe tajiri au upone malaria mkuu.
Naona Bora wangeanza kukuombea upone malaria maana malaria ndiyo inakufanya uone wamevaa yebo yebo.
 
Wanatembea viatu mbele vimetoboka
Ungewaambia wajiombee kwanza wenyewe ili waupate huo utajiri.!!

Shida kubwa za hawa ndugu zetu ni hizi;

1. Wanajiona wao ni jirani wa Yesu. Yaani pale Galilaya, toka kwa Yesu hadi kwao, ni nyumba hii na hii..!!

2. Wao ndo wanarogwa sana. Wana maombi ya kuondoa virogo

3. Wao ndo wana mapepo ya hatari

4. Wao ndo wana laana za ukoo
 
Vita uliyoanzisha na waliookoka , WATAKATIFU, watu Bora, huwezi vita hiyo.

Baba Yako shetani amewashindwa sembuse wewe?
 
Sisi hatuna fedha tena wala dhahabu, hila tulichonacho ndio tunakupa. Kwa jina la Yesu POKEAAA!

Mambo ya imani yanakutakaa uwe submissive usiwe mtu wakuhoji hoji sana kwa sababu majibu yatakuja bila logic yoyote ya kibinadamu.

Sema Aimeen!
 
Hakuna kitu kibaya kama kupima mambo ya kiroho katika mwili
Hii inaonesha ulivyo mjinga na kipofu
Kama hua unasoma maandiko
Watu waliokua wanaombea na kutoa Baraka walikua wa kawaida
Mfano ni Mfalme Sauli alipakwa mafuta na Nabii Samuel na kua Mfalme wa Israelites,
Vile vile ndie akaja kumpaka mafuta ya ufalme Daud
Angalia watu kama Nabii Eliya,Yona,Elisha,Yohana hata Yesu mwenyewe walikua ni watu maskini kwa mtazamo wa nje wa kibinadamu ila ndani walibeba ujumbe wa Kiungu wenye nguvu kubwa,

Hivyo kudharau watu ambao wanakuja kukuombea jambo ambalo wao hawana ni wajibu na hakuwazuii kufanya hivyo ati kwa sababu ni maskini la hasha hapa Duniani kuna watu hua wanakufanyia maombi bure na hata haujui ikiwemo wazazi wako na watu usiowajua wewe
Hivyo ndugu yangu badilisha mtazamo aisee hii imekaa vibaya!
 
Back
Top Bottom