KERO Walimu ajira mpya Halmashauri ya Msalala-Kahama hatujalipwa pesa ya kujikimu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Naomba tusaidie kupaza sauti huenda mamlaka zikasikia kilio chetu tukasaidika.

Sisi walimu ajira mpya intake ya March-July 2025 kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Msalala hatujalipwa pesa zetu za kujikimu mpaka sasa na tukifatilia tunapewa majibu yasiyoridhisha.
 
Wapo hapa watawasikia na kulifanyia kazi hilo!, hebu waje.
 
Sasa hii si waandikie watu wenye mamlaka ya suala hili
 
Tulieni vijana.Tumezibadilishia matumizi.Bajeti hii mtakumbukwa watoto wazuri.Uvumilivu nao ni ukubwa mjue!
 
Mshahara si unapata? Tuombee na sisi majobless tupate kazi
 
Acheni kuleta taharuki, amani na haki (pesa za kujikimu) kipi muhimu?
 
Weka jina lako tukulipe
 
Amani kwanza haki itafuata teacher.Msalala ni wilaya ndani ya mkoa wa Shinyanga sasa Kahama hapa ni kiunganishi au vitu gani?(unafeli wapi ticha).

Ingia machimboni huko Nyakagwe,Buly,Nyamishiga,Ngula ukatafute dhahabu utakuja kunishukuru badae
 
Halimashauri inaongozwa na kibaka Rose Manumba, wanachojua ni kuiba tu.

Hii halimashauri ni useless kabisa, huduma mbovu aswaa nilikuja uko nilipopata rikizo ya Tanzania,,aisee it is rubbish
 
Nyie si mliona walioandamana malofa mkashiriki na kujaza kura za veggies, haya pazeni sauti wenyewe..!!

Na kumaniner zenu msilipwe mpaka maji muite mma
 
Tangu Aprili 2025, tumekuwa tukiahidiwa na viongozi wetu kuwa posho zetu zingelipwa muda wowote. Hata hivyo, hadi sasa Julai 2026, hatujalipwa hata sehemu ya posho tunazodai.

Tunawaomba viongozi husika watuzingatie ili nasi tupate haki yetu ya malipo ya posho, kama ilivyofanyika kwa waajiriwa wengine ndani na nje ya Halmashauri ya Wilaya ya Msalala.
 
Tunaomba Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI itusaidie kufuatilia suala hili.

Sisi walimu walioajiriwa mwaka 2025 katika Halmashauri ya Msalala, Wilaya ya Kahama, Idara ya Elimu ya Sekondari, bado hatujalipwa fedha za kujikimu hadi sasa.

Tunafahamu kuwa halmashauri nyingi nchini zilipokea fedha kutoka Hazina mwezi Julai na tayari zimelipa watumishi husika. Hata hivyo, Halmashauri ya Msalala bado haijatoa malipo wala maelezo ya kuridhisha kuhusu kuchelewa huko.

Tunaomba mamlaka husika zifuatilie suala hili na kuhakikisha tunalipwa stahiki zetu kwa wakati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…