Walimu ambao tumeajiriwa na Serikali mwaka huu tutalipwa mshahara?

Walimu ambao tumeajiriwa na Serikali mwaka huu tutalipwa mshahara?

Mpenda kazi

Senior Member
Joined
Dec 13, 2013
Posts
178
Reaction score
104
Habari wadau?

Nimekaa nakutafakari mwenendo wa serikali yetu hii tokea mwaka huu 2015 ulipoingia. Mwanzo kabisa walikuwa wakisua sua kutuajiri kwa kile kilichoelezwa kuwa serikali haina pesa za kutosha.

Haya sawa mara ilipofika tareh 27 april wakaamua kutuajiri kwa mizengwe zengwe hivyo hivyo. Wakatuambia turipoti halmashauri kuanzia tareh 1 May - 9 May.

Tukaripoti, lakini cha ajabu wao walituahidi kuwa fedha za kujikimu tutazikuta hukohuko yaani zimeshatumwa. Sote tunafahamu katika halmashauri nyingi hakukuwa na fedha bali halmashauri zenyewe zilitoa fedha kutoka katika vyanzo vyake.

Ndio mkaona baadhi wamepewa hela za siku tatu, wengine siku nne, wengine nusu ya hela na wengine wakapewa zote japo bado fedha za mizigo hazijatolewa. Na wengine hawajapewa kabisaaa......

Na mbaya zaidi serikali ipo katika kipindi cha bajet, kipindi ambacho serikali huwa inajifanya kubana sana matumizi hadi hapo bajet zake zitakapopitishwa....

Wanafunzi wa vyuo vikuu wanagoma mikopo yao hawajapewa.....

Sasa najiuliza kwa mizengwe hiyo sisi walimu wapya tutapata mishahara ya mwezi huu kweli?

Naomba pia kwa wale waoefu watujuze.

Asanteni
Naomba kuwasilisha......
 
sio mwaka huu tu wa mwaka jana nao hvyohvyo tu
 
Mpaka wakakupa ajira jua wanauwezo wa kukulipa.
Inshubinaweza ikatokea wenzako wakapata wewe ukacheleweshewa.
 
Serikali ina hela kupita maelezo. Utalii, madini, gas, kodi, misaada, mikopo, nk
 
Mshahara hauchelewi na mwezi wa 7 utatoka uswaze
 
Mkuu naomba kukuhakikishia kuwa mshahara wenu utaingia kama kawaida bila usumbufu wowote na tena kwa mwaka huu wa uchaguzi ndio kabisaa...nakumbuka mwaka 2010 mbali tu na kuweka salary ile tu baada ya budget waliongeza mshahara kwa asilimia kubwa

Na ndio maana siku hizi lawama zilizopo ni wale waalimu wanaohitaji pension zao ila si kukosa mshahara. Usiogope na wala usikatishwe tamaa,kwenye ualimu ukitulia vizuri utafanya mambo makubwa sana in a short time ilimradi tu uwe na mipango.
 
Nashukuru sana mkuu kwa ufafanuzi uliojaa busara na hekima za hali ya juu. Ni wachache sana walinielewa katika maelezo yangu.
 
Inategemea km uliingia kwenye payroll kabla ya tarehe tisa utapata wa mwezi huu ambapo ni wachache sana ila mwezi wa 6uhakika.
 
Mimi Headmaster wangu kaniambiaa sisi tulioajiriwa...mwaka huu mshahara wetu utatoka kama kawaida ila wengi tutapokelea Halmashauri hadi mifumo yao ya ulipaji katika benki zetu itakaa sawa...kikamilifu maana.....watu ni wengi na wengi wetu tumefungua ma akaunt Nmb juzijuz...tu
 
Back
Top Bottom