Walimu Hisabati na kiingereza wapewa mafunzo Dodoma

Walimu Hisabati na kiingereza wapewa mafunzo Dodoma

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Katibu Tawala Msaidizi wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi mkoani Dodoma, Vincent B. Kayombo, amefungua mafunzo ya siku mbili kwa walimu wa Kiingereza na Hisabati katika wilaya ya Kondoa. Mafunzo haya yameandaliwa kwa ushirikiano na Mradi wa Shule Bora, unaolenga kuboresha elimu nchini.

Kayombo amepongeza juhudi za Shule Bora na kueleza kuwa, licha ya Mkoa wa Dodoma kufanya vizuri katika mitihani ya Taifa, bado kuna changamoto katika masomo haya. Ameeleza kuwa mafunzo haya yatawawezesha walimu kuboresha mbinu za ufundishaji na kuinua viwango vya ufaulu.

Aidha, amewataka walimu kutumia mafunzo haya kwa umakini na kuhakikisha wanayawasilisha kwa wenzao baada ya kurejea mashuleni. Mradi wa Shule Bora, unaofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia UK Aid, ulianza mwaka 2021 na unatekelezwa katika mikoa tisa kwa lengo la kuimarisha elimu nchini.
 
Back
Top Bottom