Wakubwa hebu shirikisheni bongoz enu kwenye hili jambo.
Kuna wafanyakazi hewa wengi sana na kulipa mwezi mmoja dirishani ni njia mojawapo ya kuwabaini.
Heko serikali kwa hatua hii.
OTIS
Kuna orodha ya wafanyakazi wote (walimu) na vituo vyao vya kazi vinajulikana! Kama hatuwajui huyo cashier atawajuaje, ? maana vitambulisho kila mtu anaweza kutengeneza. Labda watakuwepo watu hawa wote ili kumtambua kila mtu kwa sura yake.
[*]cshier
[*]head-ticha
[*]mratibu
[*]afisa elimu (msingi + sekondari)
[*]mkurugenzi + afisa utumishi + mwanasheria
[/LIST]
Je hawa watu hawana kazi nyingine muhimu ya kufanya? Je anayepeleka hiyo orodha ya watumishi hewa ni mani miongoni wma hawa?
Tukiwa tunasherehekea miaka 0.5karne, hili linaturudisha miaka ya 47!!!
Pole sana hujui ulisemalo,......
Na ndio maana kuna fikira za kijinga, hivi unaweza kukubaliana na mtu anaekwambia 1 + 1= 3? ukikukubaliana na huyu basi wewe ndio utakuwa mjinga zaidi kuliko yeye.Kumbukak mi sifikirii pamoja na wewe. Kila mtu anafikira zake.
Yaani kweli sie tunazidi kusonga kinyuma nyuma! Hiyo headache ya kupanga mstari nmb kuchukua hela haijatosha, sasa ni dirishani? Na hao wanaolipa na mabosi wao inabidi wavalishwe ile chuma ya maksai ili wasitafune hizo za walimu hewa!
Kulipa dirishani kutabainisha vipi hao wafanyakazi hewa,nani anayewajuwa wafanyakazi wote kwa sura zao.Wakubwa hebu shirikisheni bongoz enu kwenye hili jambo.
Kuna wafanyakazi hewa wengi sana na kulipa mwezi mmoja dirishani ni njia mojawapo ya kuwabaini.
Heko serikali kwa hatua hii.
OTIS
Kulipa dirishani kutabainisha vipi hao wafanyakazi hewa,nani anayewajuwa wafanyakazi wote kwa sura zao.
Nataka wanaJF mtambue kuwa uhakiki huu unahusu sekta zote za umma. Kwa taarifa nilizo nazo ni kwamba watumishi watapewa HUNDI baada ya mtumishi kuwasilisha (yeye mwenyewe na si kutuma mtu) vitu vifuatavyo:-
I. Kitambulisho cha kazi chenye picha.
II. Salary slip za hivi karibuni.
Kadhalika watumishi waliopo masomoni na wagonjwa wa muda muda mrefu wapewe taarifa ili wawepo siku hiyo. Ambaye hatakuwepo atahesabika kuwa ni mtumishi hewa na hundi yake itarudishwa hazina na yeye kufutwa.