Walimu kugoma baada ya mwezi mmoja wasipolipwa malimbikizo yao yaliyofikia bilioni 33....

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT), kimetoa mwezi mmoja kwa serikali kulipa malimbikizo yao ya madeni ya walimu yanayofikia bilioni 33.







Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, rais wa chama hicho, Greisoni Mukoba, alisema wamechoka kupewa ahadi hewa na serikali ndio maana wamefikia hatua hiyo.


‘Tumetoa mwezi huu wa tisa uwe wa mwisho kuililia serikali, baada ya hapo tutaamua hatua gani tufanye, maana tumekutana na makatibu wakuu wa wizara zinazowahudumia walimu lakini bado tunaishia kupewa ahadi hewa,” alisema Mukoba.


Mukoba aliongeza kuwa Agosti 14, mwaka huu, walikutana na makatibu wakuu wanaowahudumia walimu pamoja na Katibu Mkuu ofisi ya Rais Menejimenti ya Umma, wakatakiwa kuwasilisha madai yao yote.


“Tulikutana na makatibu, katika kikao hicho, tuliwafahamisha kuwa walimu wanaidai serikali zaidi ya sh bilioni 33 na mwisho wa kikao hicho tulikubaliana CWT iwakilishe madai hayo ndani ya wiki mbili,” aliongeza Mukoba.


Mukoba alisema wiki mbili zilipofika, walienda kuonana tena na Katibu Mkuu, ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na kuwasilisha vitabu vyenye madai mbalimbali ya walimu.


“Madai hayo tuliyaambatanisha kwenye barua Na CWT/004/UTMS/VOL.11/94 na madai hayo sasa yamefikia sh bilioni sita,” alisema Mukoba.

Mukoba aliishangaa serikali kuanzisha Mpango wa Matokeo Makubwa sasa “Big Result Now”, huko walimu ambao ndio watekelezaji wakubwa wa mpango huo, wana maisha magumu kutokana na mishahara kuwa midogo na kuzidi kwa malikimbizo ya madeni yao.


“Walimu ambao ndiyo watelekezaji wakuu wa mpango huu japo hawaelewi au hawajapewa semina elekezi, lakini ndio watekelezaji wakubwa.

Naishangaa serikali kuwadharau walimu na nakuhakikishia mpango huo hautafanikiwa kama walimu hawapati haki zao,” alisema Mukoba.


Mukoba aliionya serikali ikamilishe madai ya walimu ili wafanye kazi kwa moyo tofauti na sasa ambapo wengi wamekata tamaa.


‘‘Walimu wa nchi hii wamekata tamaa. Mioyo yao imekufa ganzi kwa sababu serikali imekataa kuwalipa malimbizo yao.

Kwa nini serikali imeamua kuwatendea jeuri walimu kiasi hiki?” alihoji Mukoba.


 

hizi chokochoko na vijana wanajiandaa na mitihani ngoja tuisubiri hiyo BRN
 
Watagoma kufanya nini? Kuendesha bodaboda? Maana naona baadhi ya Waalimu wa Shule ya hapa kijijini ni madereva wa bodaboda walizonunua kutokana na mikopo ya NMB waliyokopa kwa udhamini wa Serikali!
 
Kugoma sio mpaka mkoba atangaze sisi tunaojua jinsi serikali ilivyotutenga tulishaga goma zamani. ila viela vyao tunavichukua na kuongeza kwenye maisha mengine. Sasa hivi kuna BIG RESULT na EQUIP (kufundisha wakufunzi kingereza) Hivi vitu kwa uhakika haviwezi fanikiwa kwa sababu watu wanaganzi za kufa mtu moyoni.
 
Big result now without big salary now is the big problem now....
walimu kwa mikwara mmh!!!!
cc Baba V
 
Last edited by a moderator:
Big result now without big salary now is the big problem now....
walimu kwa mikwara mmh!!!!
cc Baba V

Mimi hiyo wanayoiita BRN sina hata haja ya kuhangaika nayo..... nawaangalia tu wanavyocheza cheza na vikauli vyao hivyo...
 
Mimi hiyo wanayoiita BRN sina hata haja ya kuhangaika nayo..... nawaangalia tu wanavyocheza cheza na vikauli vyao hivyo...

Hata mi sina haja nayo ila nina haja na vihela vya semina ya BRN tu.....
 
Wakati wa mitihani umekaribia, na ndo siraha kubwa waliyonayo walimu!
 
Mimi hiyo wanayoiita BRN sina hata haja ya kuhangaika nayo..... nawaangalia tu wanavyocheza cheza na vikauli vyao hivyo...

Kilimo mwanza, sorry Kilimo kwanza, mkukuta, mkurabita, nguvu mpya kasi mpya, mtaji wa masikini.. na BRN. Hakuna iliyofanikiwa hata moja!
 
Wagomee!! Wanajeuri hiyoo? Wagome waone cha mtema kuni, tutafuta ajira zao zote na kuagiza walimu wengine toka nchi jirani na hata nchi za mbali, tanzania haiongozwi kwa vitisho vya waajiriwa, wafanye kazi na si huu ulimbukeni wao na viongozi wao uchwara, dola itatumika
 

Bado umelewa....?
 
Watagoma kufanya nini? Kuendesha bodaboda? Maana naona baadhi ya Waalimu wa Shule ya hapa kijijini ni madereva wa bodaboda walizonunua kutokana na mikopo ya NMB waliyokopa kwa udhamini wa Serikali!

Sio kila thread lazima uchangie.
 
Teh! teh teh teh!..hv kumbe kuna watu wanaamn Mkoba asemayo..njoo na data kwanza ni ngoma gani alishaundaa mkafanikiwa??
 
Mgomo upi tena jamani???? Mbona wengine tumegoma toka kitambo.!!!!!!!?????
 
Hii ndo bongo bhana aka shamba la bibi. Ujanjaujanjaaaa mwingii ilimradi siku zinasonga chzea BRN ww.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…