Walimu mnaosubiri kuajiriwa na serikali msisahau kukariri wimbo huu

Walimu mnaosubiri kuajiriwa na serikali msisahau kukariri wimbo huu

Joined
Aug 1, 2013
Posts
89
Reaction score
11
Workers' Solidarity Songs

Solidarity Song;

Solidarity forever,
Solidarity forever,
Solidarity forever,for the union makes us strong.

In Swahili:
Wimbo wa mshikamano

Wafanyakazi wote tujiunge pamoja,
Wafanyakazi wote tujiunge pamoja,
Wafanyakazi wote tujiunge pamoja, kujitenga hatari.
Haya shime tujiunge, haya shime tujiunge,
Haya shime tujiunge, kujitenga hatari.

Solidarity for teachers' power forever.
Mshikamano, daima ndio ukombozi wetu.


Kauli za mshikamano
(i) Kiongozi: Teachers
(ii) Wote: Shaping the future.
(iii) Kiongozi:Walimu,
(iv) Wote: Nguvu moja, sauti umoja
(v) Kionozi:Teachers
(vi) Wote: A force for social change

WIMBO MAALUM WA CWT
1. Chama cha Walimu, Tanzania moto moto
Chama cha Walimu, Tanzania CWT
Hulinda haki na Maslahi ya Walimu Nchini
Husimamia Maadili mema ya Walimu Tanzania
Chama chetu Imara tena ni thabiti.

Kiitikio

(Tuungane) Tuungane walimu wote nchini tuungane x 2
Mshikamano daima x 2
Mshikamano walimu ni Mkombozi wetu
Tufanye kazi kwa moyo x 2
Tufanye kazi kwa moyo, tujenge Taifa letu la Tanzania x2

2. Chama cha Walimu ni dira ya Walimu
Moto wetu wa Chama ni WAJIBU NA HAKI
Ni kiungo cha Walimu wote nchini Tanzania
Husuluhisha migogoro yote ya Walimu nchini
Husuluhisha migogoro yote ya Walimu nchini
Chama chetu Imara tena ni thabiti

Kiitikio

3. Chama cha Walimu Nchini Tanzania
Ni chama Imara na chenye Msimamo
Kinajenga Mahusiano mema na Vyama vingine
Kinashirikiana na vyama ndani na nje
Chama chetu Imara tena ni thabiti
Kiitikio

WIMBO WA UZALENDO
Tanzania, Tanzania, Nakupenda kwa moyo wote,
Nchi yangu Tanzania, Jina lako ni tamu sana,
Nilalapo nakuota wewe, Niamkapo ni heri mama wee,
Tanzania, Tanzania, Nakupenda kwa moyo wote.

Tanzania, Tanzania, Ninapokwenda safarini,
Kutazama maajabu, Biashara nayo makazi,
Sitaweza kusahau mimi, mambo mema ya kwetu kabisa,
Tanzania, Tanzania, Nakupenda kwa moyo wote.

Tanzania, Tanzania, Watu wengi wanakusifu,
Siasa yako na desturi, Ilikuletea uhuru,
Hatuwezi kusahau sisi, Mambo mema ya kwetu hakika,
Tanzania, Tanzania, Nakupenda kwa moyo wote
 
Walimu ndio mliotucheleweshea ukombozi wa pili wa Taifa hili.Kelele nyiingi mkipangiwa kusimamia chaguzi mnaufyata!Hopeless Cheaters!
 
Walimu ndio mliotucheleweshea ukombozi wa pili wa Taifa hili.Kelele nyiingi mkipangiwa kusimamia chaguzi mnaufyata!Hopeless Cheaters!

Very true...
tatizo walimu wengi wanatumia vyeti vya mashangazi na mashemeji ukimwambia swala la kugoma
ni sawa na kumpa mtihani tena wa necta.
 
Back
Top Bottom