Kulwa Paschal Martin
Member
- Apr 20, 2024
- 25
- 26
UTANGULIZI.
Walimu wamekuwa chachu na msaada mkubwa sana katika taifa letu, kwani wao ndiyo daraja la mafanikio ya watu wengi, tunakubaliana kuwa, walimu wamekuwa kama wazazi/walezi wetu na kuna muda wanachukua jukumu la kutuwajibisha ili kuhakikisha tunakuwa watu bora zaidi katika jamii.
Katika mikakati ya kuboresha mfumo wa elimu, ni muhimu sana kuwaangalia kwa jicho tofauti na kuwajali walimu ili walau kuwapa motisha na kuhakikisha wanakuwa na furaha, pia katika kuhakikisha wanafanya kazi katika mazingira mazuri na shawishi ili kuboresha utendaji wao, kwani kama wao wanafuraha ni rahisi sana kufanya kazi kwa moyo wote..
Mfano. kuna mwalimu mmoja toka kigoma, maarufu kama mwalimu YUFRESH (Yusuph Ibrahim), Amekuwa kivutio/Hamasa kubwa sana kwa wanafunzi na hii imepelekea hamasa kubwa kwa wanafunzi kwenda shule na kujenga fikra kuwa, kusoma ni furaha sio adhabu na hii inachochea kasi ya wanafunzi kupenda shule (Kupenda kusoma). Tufikirie hivi, kama tukiwa na walimu mfano wa mwalimu YUFRESH, kila shule tutakuwa tumekomboa wanafunzi wangapi?? na kuwafanya wapate hamasa ya kusoma na kuona kuwa elimu ni furaha sio adhabu??. Wanafunzi, hasa wa shule za msingi na sekondari bado wana dhana kuwa kusoma ni adhabu sio kupata maarifa na mkombozi wa maisha yao ya baadae na hii husababishwa na jinsi walimu wanavyo watendea wanafunzi kwa kudhani adhabu ya viboko ni kama kumfundisha (kumuwajibisha) mwanafunzi ila kiuhalisia viboko havitoshi kwani kuna wakati mwalimu anahitaji kukaa na mwanafunzi na kuhojiana nae, kwa kufanya hivyo inaweza kupelekea mwalimu kujua vitu vinavyomkabili mwanafunzi na namna ya kumsaidia zaidi ya viboko.
View: https://www.youtube.com/watch?v=ABoBWjyzMRo
View: https://youtu.be/rOWBH6HZ-Sw?si=Fl0GqqHEbH1cJ3X0
View: https://www.instagram.com/reel/C8E_K6lsXAx/
Kuna namna kama taifa tunahitajika kufanya juhudi za kimakusudi (Juhudu za ziada) ili kutoa hamasa kwa walimu. Sekta ya walimu imesahaulika kwa namna fulani, ila bado tuna nafasi ya kuhakikisha tunawapa furaha na hamasa zaidi katika utendaji.
MAMBO YA KUFANYA ILI KURUDISHA FURAHA YA WALIMU TANZANIA.
Mambo yafuatayo yakifanyika kiusahihi, yatachochea hamasa kwa walimu, na hii itaathiri mpaka maendeleo ya wanafunzi, kwani kuna mstari mwembamba sana kati ya furaha, ridhiko la mwalimu na maendeleo ya mwanafunzi.
01. Kuanzisha TUZO za walimu kitaifa. (Tanzania Teachers Awards).
Nadhani tunaona kuwa, karibu kila sekta kuna namna wanajipongeza kwa kutambua wafanyakazi wanaofanya vizuri ila hakuna tuzo au cheti cha pongezi kitaifa, kutambua na kuthamini juhudi za walimu Tanzania. Napendekeza kuanzishwa kwa tuzo za kitaifa ambazo zina thamini na kuelewa mchango wa mwalimu katika sekta ya elimu na tuzo hizi zinaweza kuwa na vipengele kama (Mfano):-

- - Mwalimu bora kwa kila somo.
- - Mwalimu mkuu bora kila mkoa.
- - Shule bora kila mkoa.
- - Mwalimu wa taaluma bora.
- - Mwalimu wa michezo bora.
Kwa kufanya hivi ni kuchochea na kuipa sekta ya elimu taswira ya ubora na ufanisi zaidi, Itawafanya walimu wajione kuthaminiwa sana. Chama cha walimu Tanzania (CWT), kinatakiwa kuwekeza nguvu huku wizara ya elimu ikisimamia mchakato mzima.
02. Kuipa thamani sekta ya elimu (Walimu).
a.-Kuongeza mishahara ya walimu. Hiki kimekuwa ni kilio cha muda mrefu cha walimu na hapa tunaweza kuona vile walimu wamekuwa wahanga wa mikopo, sababu ya mishahara na maslahi kuwa madogo. Watu kuona kuwa taaluma ya ualimu ni kama kuzika ndoto. Nadhani hapa serikali inatakiwa kukaa na chama cha walimu Tanzania (CWT) ili kufanya tathimini ya mishahara ya walimu na kuona namna ya kuongezeza maslahi/Mishahara na kutatua changamoto zote zinazo wakabili walimu, kwa kufanya hivi ni kuipa thamani sekta ya ualimu Tanzania.
b.-Kutoa elimu ya kujiajiri/Ujasiliamali kwa walimu. Kutokana na wimbi la walimu kuwa wahanga wa mikopo (MIKOPO KAUSHA DAMU) na maisha magumu kuna umuhimu wa CWT, kuwa na semina na uhamasishaji kwa walimu ili kuwawezesha kupata maarifa ya namna wanavyo weza kujiajiri zaidi ya kutegemea mshahara ili kuinua kiwango cha uchumi kwa walimu na kuleta taswira nzuri ya elimu kwa Tanzania na namna ya kuepuka mikopo inayowaumiza kwa kuzingatia mashariti ya mikopo ili baadae isiwe miiba katika maisha yao.
c.-Kuboresha mazingira ya kazi kwa walimu. Mfano, Mwalimu mmoja kufundisha kwa kadri ya uwiano, ili kuepusha kumtumia mwalimu zaidi ya uwezo wake (Overdoze). Kama mwalimu atafundisha kwa uwiano kwa wanafunzi hii itaongeza ufanisi wa kufundisha.
Wizara ya Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) inaeleza kuwa uwiano sahihi kwa shule za msingi ni mwalimu mmoja kwa wanafunzi 40 (1:40). Uwiano kati ya mwalimu na wanafunzi umekua ni moja ya kigezo kikubwa katika kutathimini kiwango cha ufaulu wa shule husika ambapo kwa miaka mingi, shule zenye uwiano mzuri zimekua na kiwango kizuri cha ufaulu kuliko zenye uwiano mbaya. Chanzo: Gazeti la Mwanachi.
Chanzo: Gazetila Mwananchi
d.-Kutoa Motisha kwa walimu wa maeneo ya vijijini. Walimu wengi pindi wakichaguliwa kwenda kufundisha maeneo ya vijijini wamekuwa wakikimbia na kuomba kuhamishiwa mjini. Napendekeza serikali kutoa motisha ya fedha mbali na mshahara ili kuwapa hamasa walimu kubaki kijijini na kuona ni maeneo rafiki kwa ajili ya kufundisha, lakini pia kuwajengea walimu nyumba hasa kwa maeneo ambayo sio rafiki kwa makazi ya walimu.
03. Kuhamasisha wadau wa elimu katika kujali na kusaidia sekta ya elimu.
Majukwa kama Jamii forum na majukwa mengine yanaweza kuwa na kampeni za kuwahamasisha wadau wa elimu kupenda na kusaidia sekta ya elimu ili kuinua kiwango cha elimu. Kuhamasisha watu kupenda kuzitembelea shuke walizosoma, kurudi na kuzitembelea ili kuona sehemu yenye udhaifu na kusaidia. Mfano, Nakumbuka 2012, Dr. Harrison Mwakyembe alifika shule ya milambo High School (TABORA) na alihamasisha watu wote waliosoma pale wafanya jambo kwa ajili ya shule ya milambo na hii ilisaidia kurekebisha miundombinu ya shule. Tunaweza kujifunza kitu hapa pia.

HITIMISHO.
Bado tuna nafasi ta kurekebisha mfumo wa elimu na kurudisha tabasamu kwa walimu/sekta ya elimu kwani wanatuhitaji sana. Tusiiachie serikali peke yake katika kuwajali walimu/sekta ya elimu, ila kila mmoja ana wajibu katika hili, Kwani Tanzania ni yetu sote.
"Mwalimu Tabasamu Tena"
Upvote
0