KERO Walimu tulioajiriwa Januari Halmashauri ya Mkalama hatujalipwa fedha za kujikimu wakati idara ya afya wamelipwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Walimu tulioajiriwa mwezi Januari mwaka huu hadi sasa tumefikisha miezi minane bila kulipwa stahiki za fedha za kujikimu.

Tunaomba JamiiForums itusaidie kupaza sauti yetu ili kilio chetu kifike kwa wahusika. Wakati watumishi wa afya walioajiriwa kipindi kama sisi tayari wamelipwa stahiki zao, walimu bado tunasubiri bila maelezo.

Tunaomba TAMISEMI, hususan Idara ya Elimu, itusaidie kulifuatilia suala hili na kuhakikisha tunalipwa stahiki zetu kwa wakati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…