Walimu tunanyimwa ruhusa tusisome bagamoyo na tunateswa

BUMIJA

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2011
Posts
5,950
Reaction score
11,295
Mimi niliajiriwa mnamo 2008 Katika shule ya sekondari Matipwili km100 Kutoka Dar na ni Karibu na hifadhi ya saadani.Mnamo mwaka2011 mwezi wa5 nikaomba chuo,Mana kwa Pale Matipwili ilikua zamu yangu nikasome,Mnamo mwazi wa7 DEO Sekondari alipoona naenda kusoma Akaona anihamishie Moreto Sekondari Lugoba.Mwezi wa10 nikapata chuo ila DEO Akaniambia airisha mwaka lakini nilikwama.Akasema hapa chagua kazi au masomo,Kwa kua lengo langu nika some niliandika barua kwa mkuu mpya Mwl Justine Lyamuye na akapitisha ila Bado DEO akakataa.Me nikaenda chuo mana Diploma kwangu ilikua bado,wakanikatia mshahara,Nikawa nakula mara moja kwa siku, nakula mikate iliyochacha ili siku ziende.Mda mwingine naumwa natumbo naharisha na siku inapita.Nikawaeleza Cwt lakini hadi leo hawakufanya lolote.Kwa sasa nipo 2year na Nimezoea maisha hayo.Kama kuna anaeweza kunishauri mana nilifanya kazi maporini miaka4 lakini nimenyimwa haki zangu..Ualimu nimetokea kuuona Mavi kutokana na unyama niliofanyiwa.0712336687
 
pole sana jipe moyo. Wengi hawapendi kuona unafanikiwa kwa kuogopa kupokonywa viti vyao maana wengine wako maofisi c kwa taaluma bali kujuan
 
Pole sana,ualimu sio kazi,ww fikilia ulikuwa polini bado unafanyiwa unyama.Nawashauri mtakao pangwa polini mkatae.
 
Palikua hapafiki mabasi,ni bodaboda juu ya Reli,miaka4
 
Nauliza hivi CWT chama cha walimu au wasaniiiiiiiiii
 
Ila DEO wanawaonea sana waalimu wanaotaka kujiendeleza,hasa ukizingatia utawqazidi elimu ndio kabisa wanakukatalia,nakumbuka kisa cha Mwl Mmoja aliamua kuondoka hivyo hivyo wakamfuta ajira wakasema ni mtoro kazini ila aliamua kusoma na sasa ana Masters yake ameajiriwa kwenye mashirika ya NGO
 
alikukufanyia unyama wakati wewe mwenyewe ulikuwa porini na wanyama, mbona ni mulemule tu, naona hajakosea. kukubalikwako ndio maana ulistahili kufanyiwa hivyo
 
Sijapewa barua yoyote hata ya kusimamishwa mshahara
 
Pole sana inabidi ukomae na maamuzi yako kama yana manufaa mbele ya safar

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Nenda kwa walio juu ya DED ikiwa vipi nenda hata ngazi za juu zaidi.
 
Kwa DED sijaenda
Kumbe malalamiko yako hapa hayana msingi. Unataka kuniambia hujui kwamba ruhusa haitolewi na DEO bali inatolewa na DED? Hata ningekuwa mimi DEO ningefanya hivyo....Someni vizuri sheria na kufuata channel za uongozi, hapa JF tunafurahishana tu, huwezi kupata kitu.Shauri yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…