Mr Equalizer
JF-Expert Member
- Dec 14, 2013
- 611
- 727
Hakuna asiyefahamu kuwa idadi kubwa ya Watanzania ni watu maskini sana hasa maeneo ya vijijini.Serikali imejenga shule za sekondari katika maeneo mengi ya vijiji hivi kwa lengo la kuwasaidia wananchi hawa somesha watoto wao.Nikiwa kama mdau wa elimu nimeona na kusikia mambo mengi ya kusikitisha sana kutoka katika shule hizi za kata.Kwanza shule hizi zimejaa michango mingi sana kiasi cha wazazi wengi masikini kushindwa kulipa machango hiyo.mf shule moja ambayo leo sitaitaja mwanafunzi anapaswa kulipa kiasi cha tsh 200000 ili aweze kuanza kidato cha kwanza ,kiasi hiki ni kikubwa sana kwa wazazi wengi wanaopatikana maeneo ya vijijini.Baadhi ya walimu wamekuwa wakiwacharaza watoto hawa maskini viboko vya kutosha eti kwa kuwa hawajalipa michango hiyo.Mbaya zaidi walimu hawa ambao nao walisoma katika mazingira ya umaskini wa kunuka wamesahau na kuamua kuwafukuza watoto hao mpaka pale watakapokamilisha michango. Mwalimu mmoja wa shule ,jina nalihifadhi wilayani Musoma aliwaambia wanafunzi waliokuwa wamefaulu kidato cha pili kwenda kidato cha tatu kuwa ,kila mwanafunzi anapaswa kulipa kiasi cha sh 5000 ili aweze kupata matokeo yake je? ndugu walimu huu sio usaliti kwa watanzania.Tubadili tabia zetu.