Walimu tusiwasaliti watanzania shida zao ni zetu

Mr Equalizer

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2013
Posts
611
Reaction score
727
Hakuna asiyefahamu kuwa idadi kubwa ya Watanzania ni watu maskini sana hasa maeneo ya vijijini.Serikali imejenga shule za sekondari katika maeneo mengi ya vijiji hivi kwa lengo la kuwasaidia wananchi hawa somesha watoto wao.Nikiwa kama mdau wa elimu nimeona na kusikia mambo mengi ya kusikitisha sana kutoka katika shule hizi za kata.Kwanza shule hizi zimejaa michango mingi sana kiasi cha wazazi wengi masikini kushindwa kulipa machango hiyo.mf shule moja ambayo leo sitaitaja mwanafunzi anapaswa kulipa kiasi cha tsh 200000 ili aweze kuanza kidato cha kwanza ,kiasi hiki ni kikubwa sana kwa wazazi wengi wanaopatikana maeneo ya vijijini.Baadhi ya walimu wamekuwa wakiwacharaza watoto hawa maskini viboko vya kutosha eti kwa kuwa hawajalipa michango hiyo.Mbaya zaidi walimu hawa ambao nao walisoma katika mazingira ya umaskini wa kunuka wamesahau na kuamua kuwafukuza watoto hao mpaka pale watakapokamilisha michango. Mwalimu mmoja wa shule ,jina nalihifadhi wilayani Musoma aliwaambia wanafunzi waliokuwa wamefaulu kidato cha pili kwenda kidato cha tatu kuwa ,kila mwanafunzi anapaswa kulipa kiasi cha sh 5000 ili aweze kupata matokeo yake je? ndugu walimu huu sio usaliti kwa watanzania.Tubadili tabia zetu.
 
ndugu, wakati mwingine mkiitwa kwenye vikao vya wazaz hamuendi! pia kumbuka walimu wanapokea maagizo kutoka juu..nikushauri uwe unawaendea viongozi wanaohusika ikiwemo bodi ya shule! walimu ni watekelezaji tu..
 
wewe unaona hiyo laki 2 mi nyingi kwa mtoto kusoma? unatakiwa kufaham kuwa elim ni gharama tena hicho kias ni chakawaida tu
 
maisha yamebadilisha vp ulitaka watoe ada elfu 5 . hii ndiyo serikali yako kila kitu ni gharama au labda wabadili mfumo mzima wa elimu iwe bule wasichangie ata senti
 
walimu ni watekelezaji tu wa haya mambo ingekuwa ni kinyume na utaratibu wangeshachukuliwa hatua
 
Wew si mdau wa elimu ni kanjanja 2 kama wengne! Ungejua jinsi ambavyo serkal imezitelekeza shule hzo usingesema lak 2 ni kubw!
 
Wew si mdau wa elimu ni kanjanja 2 kama wengne! Ungejua jinsi ambavyo serkal imezitelekeza shule hzo usingesema lak 2 ni kubw!

Wewe inaonekana utakuwa ni miongoni mwa watu wanaoshilikiana na baadhii ya walimu kuuza vifaa ambavyo wanaviagiza kutoka kwa wanafunzi ,vifaa hivyo ni kama ;makwanja,karatasi majembe,na ndoo.Unailaumu serikali je serikali imewaagiza wafanye hivyo.Siyo kwamba sijui udhaifu wa serikali ya ccm katika kuzihudumia shule hizi.Lakini je walimu watakuwa na tofauti gani na serikali ya ccm kama nao wataendelea kuwahujumu wananchi maskini kwa ufsadi huo.Ndugu huo udokta uliupatia wapi au ulikuwa unadesa tu darasani.
 
Nimekwa mwalimu kwa muda mrefu,naifahamu sana serikali yatu kuu na utendaji wake,nazifahamu halmashauri zetu,zaidi sana nazijua bodi za shule.naomba kusema hakuna hata moja kati ya hizo taasisi inayoweza kumwagiza mwalimu auze limu, makwanja,au ndoo zinazoletwa na watoto.Nitajie halmashauri hata moja inayowaagiza walimu wawatoze pesa wanafunzi wanapotaka kujua matokeo yao ya kidato cha pili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…