waungwana naomba kwa mwenye habari ya kuaminika anisaidie kunijulisha juu ya ajira kwa walimu wa sekondary ni lini? Pia naomba mwenye kuweza nisaidia kupata shule ya kufundisha hapa mjini anisaidie contact ili ni apply kwani nimemaliza shahada ya ualimu mwezi july mpaka sasa sijapata kazi, Binafsi ni mwalimu wa kingereza (English 4 both o level and a level) na general studies au civics. jamani tusaidiane kwa hili.
Serikali imedai itaajiri walimu 23000 kwa mwaka mwaka wa fedha 2012-2013 nadhani ni mpaka mwezi wa saba ndio mwaka wa fedha wa serikali VUMILIA wanaweza kuwahi pia kuajiri
Sio wa Diploma na Digrii tu, hata walimu wa 'certificate' wanasaga lami. Hayo ndo maisha bora kwa kila mtz tena kwa kasi zaidi, nguvu zaidi, na ari zaidi!
Siyo hao tu. Namjua mtu aliyemaliza masters degree. Alikuwa mwalimu wa shule ya msingi. Huu mwaka wa pili bado anafundisha shule ya msingi wameshindwa kumpangia kazi inayolingana na elimu yake. Ndiyo Bongo. Mpaka uhonge vinginevyo wanadhani wanakukomesha wewe kumbe wanalikosesha taifa nguvu kazi.