Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,478
- 3,659
Mada inazungumzia kwa upekee uandishi na matamshi ya lugha ya kiswahili. Kingereza si lugha yetu hivyo sitalaumu sana huko. Ukiwasikiliza vijana wengi sasa unagundua hawajui hata hicho kiswahili kinachoongewa kila siku.
Nakumbuka shule ya msingi tulisoma "imla". Kwa kingereza ni dictation. Mwalimu anasoma na sisi tunaandika kwa ufasaha alichokuwa anatamka. Zoezi hilo lilifanyika hadi mwanafunzi aliweza kuandika kwa ufasaha anachotamka.
Kwa vijana wengi wa zamani ni nadra kukuta anakosea matamshi. Kinyume chake leo hii kijana aandike ujumbe kwenye status yake ya simu utaona aibu. Mfano "mwanangu una baya". Au "usimzalau usiemjua. Uyo nitajili wa kesho". Au "mungu (Mungu) si asumani" .... Na ujinga mwingine mwingi sana.
Waathirika wakubwa kwenye hili kundi ni vijana fulani hivi wa kada ya chini. Madereva, mafundi, etc. Wa kada ya juu nao tatizo halijawaacha.
Hawa walimu wanaofundisha hasa elimu ya msingi ndio hao hao waliofeli imla na hawataweza kuwasahihisha wanafunzi. Ni aibu. Inafika wakati unaona kijana wa kada hiyo kaandika kiswahili fasaha, unaanza kumshangaa. Unagundua kuwa huyu ana akili. Akili ya kuweza kuainisha. Walimu mnakwama.