Walimu wa Moshi Vijijin wanateseka

kitongoroso

Member
Joined
Nov 3, 2013
Posts
29
Reaction score
4
waalimu wa moshi vijijini wanaomba kuiuliza serikali kuwa wao ni tofauti na waalimu wengine Tanzania? mbona wanafanyiwa hivi? wananyanyasika sana kutoka kwenye idara zao za elimu, tsd, na utumishi.

Mfano waalimu waliotoka kujiendeleza kimasomo toka mwaka 2012 hadi leo hawajawabadilishia muundo wa utumishi. Wamepewa barua lakini hadi leo hawajalipwa mshahara mpya wakiuliza wanaambiwa ni hazina wanawacheleweshea. Wanauliza kuwa hazina wanaona tu halmashauri hii?

Si hivyo tu halmashauri hii haifuati kabisa taratibu zilizowekwa na serikali katika kulipa waalimu wake mfano tunafahamu mwalimu akitoka njee ya kituo chake cha kazi hulipwa kiwango flan kulinga na ukubwa wa mshahara wake ila kwa halmashauri hii kila kazi utakayopewa nje ya kituo cha kazi utalipwa shilingi elfu 3 tu huu ni unyanyasaji mkubwa.

Katika idara ya elimu afisa elimu wao hana utartibu mzuri wa kutoa promotions kwa waalimu kwani amekuwa na makengeza ya kuwapa wanawake promotions tatizo lililo mfanya ahamishwe kwenye halmashauri ya hai kwani aliiharibu sana sasa tatizo linaanza kujionyesha kwenye wilaya hii. SERIKALI MPO WAPI?
 
Hili suala ingekuwa vyema wakimtuma Mbunge wao kufuatilia iwe ni hazina au utumishi.

Poleni waalimu!.
 
Padieem elfu tatu (3), naomba kuuliza huyu mwalimu analala nje ya kazi kwa posho hii?
 
Padieem elfu tatu (3), naomba kuuliza huyu mwalimu analala nje ya kazi kwa posho hii?
 
Wengine laki tatu kwa siku wengine buku tatu. Hii nayo ni sehemu ya maisha. Mungu tusaidie.
 
Mtoa mada sahihisha kauli yako.wilaya gani ambayo walimu wanapewa stahili zao? Ndio maana unasikia malimbikizo ya walimu ni pamoja na madeni yalizopo plus arrears likizo na madeni mengine.piga kazi acha kulalamika na huu ni upepo tu utapita.tanzania nzima walimu wanadai.
 
serikali ya ccm ni sikivu sana msijali waalimu kuhusu madai yenu tutayashughulikia,kwanza ualimu ni wito pigeni kazi unalipwa kutokana na mahali kama ni mjini utapewa kiwango tofauti na kijijini.kigumu chama chetu
 
mbunge wao freeman.mbowe badala ya kuwatetea walimu wake bungeni amekomaa tu na tanganyika.. sasa sijui tanganyika ndio itakayowasaidia hao walimu. shame on you mbowe..!
 
mbunge wao freeman.mbowe badala ya kuwatetea walimu wake bungeni amekomaa tu na tanganyika.. sasa sijui tanganyika ndio itakayowasaidia hao walimu. shame on you mbowe..!

Mbunge gani wa ccm anawatetea walimu??? Acha unafiki .
 
Kwa hiyo kulalamika hapa na kulifikisha suala hilo kwa mbunge wenu nini muhimu kwanza?Mara ya mwisho kuzungunza na mbunge wenu ni lini au mnaona fashion kulalamika kwenye mitandao? Unadhani mtandao utatatua njaa zenu? Ona Kwanza mmekondaaa wakati mbunge wenu boongeee
 
mbunge wao freeman.mbowe badala ya kuwatetea walimu wake bungeni amekomaa tu na tanganyika.. sasa sijui tanganyika ndio itakayowasaidia hao walimu. shame on you mbowe..!
acha kupotosha we gamba,mbunge wa moshi vijijini ni gamba mwenzako cyril chami.
 
mbunge wao freeman.mbowe badala ya kuwatetea walimu wake bungeni amekomaa tu na tanganyika.. sasa sijui tanganyika ndio itakayowasaidia hao walimu. shame on you mbowe..!

Toa uongo mako hapa. Mbunge wao ni Cyril Chami... Mbowe yupo Hai... Tena kitu alichofanya Mbowe ni kushinikiza kuondolewa kwa maafisa wabovu wote... ndo maana Hai inapanda kila uchao. Acha upotoshaji
 
mbunge wao freeman.mbowe badala ya kuwatetea walimu wake bungeni amekomaa tu na tanganyika.. sasa sijui tanganyika ndio itakayowasaidia hao walimu. shame on you mbowe..!

Acha majungu! Mbowe ni mbunge wa Hai na sio Moshi vijijini. Mbulula ww.
 
mbunge wao freeman.mbowe badala ya kuwatetea walimu wake bungeni amekomaa tu na tanganyika.. sasa sijui tanganyika ndio itakayowasaidia hao walimu. shame on you mbowe..!
------- umeishiwa hoja maskini wa tisheti na kofia ya kijani uliambiwa mbowe ni mbunge wa moshi vijijini? Mrudishie shangazi yako cm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…