KITOMONDO
Senior Member
- Aug 2, 2012
- 100
- 20
Manispaa ya Songea ime jaa ufisadi wa hali ya juu,ambapo watendaji wake wanafanya hujuma kwa walimu wa sayansi ambao walitakiwa kuwa na semina ya kuongeza ufanisi katika taaluma yao ya ufundishaji wa masomo hayo,semina hiyo iliyo takiwa kufanyika mwezi wa nne haijafanyika hadi sasa,kumekuwa na sinto fahamu kuhusu semina hiyo kwani huu ni mwaka wa pili sasa tokea walimu wa sayansi kutopatiwa haki yao ya msingi ya kufanya semina hiyo,tokea mwaka jana walimu wa sayansi hawajapata fursa ya kufanya semina hiyo ili hali wa halmashauri nyingine wana pata haki yao ya msingi ,taarifa kutoka kwa afisa mmoja wa idara ya utumishi wa umma wa manispaa hii zinasema kuwa fedha za semina za walimu hao zime liwa na wajanja wachache wenye uchu wa kutajirika haraka, sisi kama walimu wa sayansi tuna mwomba waziri wa elimu aingilie kati suala hili ili tuweze kupatiwa haki yetu ya msingi ya kufanya semina