Walimu wa vyuo wafeli mitihani vibaya

Walimu wa vyuo wafeli mitihani vibaya

Lukolo

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Posts
5,143
Reaction score
3,199
headline_bullet.jpg
Hakuna daraja la kwanza kwa vyuo vyote
headline_bullet.jpg
Watalazimika kurudia mtihani kufikia viwango



Kawambwa-1.jpeg

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa


Wakati serikali ikisuasua kutoa ripoti ya tume ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, iliyokuwa ikichunguza matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka jana, matokeo ya mtihani wa ualimu ya mwaka huu nayo ni janga.

Katika matokeo ya mtihani wa ualimu waliofanya Mei mwaka huu ambayo yametolewa jana na Baraza la Mtihani la Taifa (Necta), wahitimu 2,906 wa ngazi ya stashahada wanatakiwa kurudia mitihani (supplementary) ndani ya miaka miwili huku wengine 533 wakiwa wamefeli kwa daraja la 0.

Matokeo hayo ambayo yametangazwa kwenye tovuti ya Necta na kusambazwa kwenye vyuo vyote vya ualimu nchini, yanaonyesha kwamba hakuna kabisa mhitimu aliyefaulu kwa kiwango cha juu (distinction), 27 wamefaulu kwa daraja pili (credit) na waliofaulu kwa daraja tatu (pass) ni 6,374.

Madaraja ya mitihani huo yamepangwa kwa distinction (sawa na daraja la kwanza), credit (sawa na daraja la pili), pass (sawa na daraja la tatu), supplementary (kurudia baadhi ya masomo) na fail (daraja sifuri)Jumla ya vyuo 139 vilifanya mtihani huo, kati yake vya astashahada ni 90 na stashahada ni 49.

Matokeo hayo yanaonyesha kwamba vyuo kama Mpwapwa yenye wahitimu 442 ni mhitimu mmoja tu aliyepata daraja pili yaani credit wakati waliofaulu kwa daraja tatu yaani pass ni 295, wanaotakiwa kurudia mitihani ni 136 na waliofeli ni tisa.

Chuo cha Marangu chenye wahitimu 1,026 daraja pili ni 7, la tatu ni 630, wanaotakiwa kurudia mitihani ni 343 wakati waliopata daraja 0 ni 38. Matokeo hayo yanaonyesha kwamba chuo cha Monduli waliopata daraja pili ni 9, la tatu ni 295, wanaorudia ni 66 na 0 ni wawili.

Chuo cha Korogwe kati ya wahitimu 1,080 matokeo yanaonyesha kwamba hakuna waliopata daraja la pili, la tatu ni 655, wanaorudia ni 328 na 0 ni 77 wakati Eckenforde hakuna pia aliyepata daraja la pili, wakati daraja la tatu 51, wanaorudia ni 21 na 0 ni 16.

Matokeo hayo yanaonyesha kwamba vyuo vya Arusha, Mtwara, Benjamin Mkapa, Dakawa, Butimba, Chuo cha Ualimu Zanzibar, Pemba Islamic na Bukoba Lutheran hakuna waliopata daraja pili.

Matokeo hayo yanaonyesha kwamba Pemba Islamic waliopata daraja la tatu ni wanne, wanaorudia ni 29 na 0 ni 19; wakati Chuo cha Ualimu Zanzibar daraja la tatu ni sita, wanaorudia ni 31 na 0 ni 16 wakati Bukoba Lutheran daraja la tatu ni 12, wanaorudia ni wanne na waliopata 0 ni watatu.

Dakawa waliofaulu kwa daraja la tatu ni 352, wanaorudia ni 124 na 0 ni 24; Mtwara daraja la tatu ni 304, wanaorudia ni 145 na 0 ni 27; Benjamin Mkapa daraja la tatu ni watano, wanaorudia ni saba na 0 ni wawili; Arusha daraja la tatu ni 14, wanaorudia ni wanane na 0 ni saba wakati Butimba daraja la tatu ni 497, wanaorudia ni 283 na 0 ni 18.

Klerruu wahitimu 227 waliofaulu kwa daraja pili ni wawili, daraja la tatu ni 175, wanaorudia ni 39 na 0 ni saba; Patandi la pili ni mmoja, daraja la tatu ni 60, wanaorudia ni 21 na 0 ni 16; Bunda hakuna hata mmoja aliyepata C, wakati daraja la tatu ni 313, wanaorudia ni 159 na 0 ni 23 wakati Morogoro mmoja amefaulu kwa daraja pili, 665 wamefaulu kwa daraja la tatu ni 274 wanarudia na 49 wanamepata 0.

Tukuyu hakuna daraja la pili na 445 wamepata daraja la tatu, 107 wanarudia wakati 12 wamepata 0. Kasulu hakuna daraja la pili, 204 wamepata daraja la tatu, wanaorudia ni 77 na 0 ni 14 wakati St. Mary's hakuna waliopata daraja la pili wala wanaorudia, daraja la tatu ni watano na 0 ni mmoja.

Matokeo hayo pia yanaonyesha kuwa katika vyuo vyote kwa ngazi ya cheti (Grade A) yaani astashahada, wahitimu 5,608 wamefaulu kwa daraja pili wakati waliopata daraja la tatu ni 17,339. Pia wapo 207 waliopata 0.

Matokeo yaliyopo kwenye tovuti hiyo ni ya jumla ya vyuo 86 vya ngazi ya astashahada ya ualimu, elimu maalum vinne, stashahada (diploma) ya ualimu vyuo 48 na kimoja cha ufundi.

SOURCE: NIPASHE

My Take:

Ina maana ule mgomo baridi unawahusu pia na wakufunzi wa vyuo, au ni baraza la mitihani limeanza kutunga mitihani migumu sana siku hizi?



 
hata hao wakufunzi nadhani wanaweza feli kama wakipewa mtihani
 
kama watu hawasomi wanategemea muujiza kila mmoja amevuna alichokipanda.
 
Mkuu walioenda vyuo vya ualimu unajua sifa zao? kama wazijua hichondo halali yao!!
SP
 
Mkuu walioenda vyuo vya ualimu unajua sifa zao? kama wazijua hichondo halali yao!!
SP
kwahiyo unataka kusema wamefeli kwa kuwa uwezo wao ni mdogo au wamefeli kwa kuwa wakufunzi nao wapo kwenye mgomo baridi?
 
mkuu niseme hivi, wanaoenda vyuo vya ualimu ni "failure" yaani ukipata D's form four na E's form six huko ndo kimbilio lao~~ Leo nenda primary schools zetu ita 3 teachers, just speak in any language any critical debatable topic in country listen and analyze you will know something on our education system.
So far we have to expect more pass from secondary schools than education institutes, that is no wonder at 100%
SP
 
kama watu hawasomi wanategemea muujiza kila mmoja amevuna alichokipanda.

2mia akili ww ucongee 2 kama unajifunza kuongea sio wote wanafel kwa kutokusome huwez jua ni magumu yepi yaliyotokea.bado hujafika apo ulipo na wala hujafaulu maisha roho mbaya tu.
 
Kama form 4 wakifeli what do u expect?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Hivi inakuaje mpaka mtu anaamua kusomea ualimu tena huu wa Grade A?ni kwamba anakua amekata tamaa na maisha yake au tatzo linakua ni nin?
 
Yawezekana pia. Maana wengine wameupgrade kutoka ualimu wa astashaada kwenda ualimu was stashahada.
Kwa hiyo nao wamefeli
 
Hivi inakuaje mpaka mtu anaamua kusomea ualimu tena huu wa Grade A?ni kwamba anakua amekata tamaa na maisha yake au tatzo linakua ni nin?
Naomba upitie prospectus za vyuo mbalimbali alafu angalia CV za malecture uone wametokea wapi,wewe ukiwa shule ya msingi ulifundishwa na mwalimu wa diploma
"Vox populi,Vox dei"
 
Kichwa cha Habari tofauti na mada,ulitakiwa usema walimu tarajali
"Vox populi,Vox dei"
 
Kwa hiyo wana Disco chuo kikuu nao wamefel form six? Tatizo hakuna taasisi moja inayosimamia elim kuanzia silabus,masomo na mitihan ndiyo maana ni vigumu kutathmin kiwango cha elimu tz.kuanzia primary had vyuo vya ualimu.
 
Tatizo ni mfumo mbovu mh.MBATIA alisema wakamdhihaki kuwa hakuna tatizo ila tatizo lipo tena kubwa mitihani inatungwa kufuata mtaala wa kuungaunga wakati wanachuo wanafundishwa kufuata syllabus na mtaala na syllabus ni vitu viwili tofauti kama chui na paka
 
Back
Top Bottom