Walimu waanza kumiminika kwenye benki yao (MCB)

moyafricatz

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2015
Posts
2,904
Reaction score
4,902
Leo mapema nimetembelea MCB bank na kujionea mabadiliko makubwa yaliyofanyika hasa ktk huduma ambazo zimeendelea kutolewa na MCB bank ktk ubora wa hali ya juu kabisa.

UKWELI KUHUSU MCB.
Mwalimu Commercial Bank (MCB) ni bank ya walimu ambayo walimu Pekee ndio wanaomiliki hisa ZAIDI YA 50% na Kiwango kidogo kilichobaki kikiwa kinamilikiwa na wadau Wengine wakiwemo PSPF.

MIKOPO INAYOTOLEWA NA MCB BANK:

Kuna Aina mbili za mikopo inayotolewa

1. Mkopo wa dharura - (Salary advance).
Mkopo huu kutolewa kwa Mwl ambaye mshahara wake unapitia MCB.

Hauna masharti yoyote. Riba yake ni 5% tu. Wale wenye dharura kabla ya mshahara hujaza form maalumu papo hapo na kupata mkopo huo, kisha fedha hiyo hukatwa mwishoni mwa mwezi.

2.Mkopo kuanzia miaka mitatu hadi miaka 7 na miezi 2 (yaani miezi 86).

Mkopo huu umegawanyika katika makundi mawili.
(a) Kwa Mwl asiyepitisha mshahara MCB anaruhusiwa kupewa mkopo wa miaka 6. (Miezi 72)

(b) Kwa Mwl au mtu yeyote anayepitisha mshahara MCB bank anaruhusiwa kuchukua mkopo kwa miaka 7 na miezi 2.(miezi 86).

VIAMBATANISHO UNAPOOMBA MKOPO.
1.Salary slip 3 za hivi karibuni.
2. Picha2 mpya za passport size.
3. Barua ya vitambulisho kutoka kwa mwajiri.
4. Barua ya ajira/ mkataba wa Kazi.
5.Barua ya uthibitisho kazini.
6.Nakala ya Kitambulisho cha Kazi.
7. Nakala kati ya hizi:
- Kitambulisho cha mpiga kura
- passport
-leseni ya udereva
-kitamblisho cha Taifa.
8.Taarifa ya Bank (bank statement) ya miezi 6.

KAMA UNAUZA DENI
9. Hakikisha unapata kwanza Barua inayoonesha unachodaiwa kutoka kwenye bank unayotaka iuze Deni hilo.
KISHA: Jaza fomu ya mkopo ya MCB.

FAIDA YA BENKI YA MWALIMU (MCB)

1. Mkopo unaupata Chini ya siku 7. (Kuanzia siku2-6).

2. Bank ya MCB ina offer ya miezi 2 zaidi ya bank nyingine zinazoishia miaka 7 tu. Na Kiwango hicho cha miezi miwili chaweza kuanzia na pesa kiasi cha 300,000/=, 500,000/= na kuendelea kutegemeana na take home yako na idadi ya miaka unayochukua mkopo huo.

3. Bank ya MCB wananunua mikopo kutoka bank nyingine. Hii ni tofauti na kipindi kilichopita ambapo walikuwa hawanunui mikopo hiyo.

FAIDA NYINGINEZO:

Bank ina Aina mbalimbali za accounts.
1. Current account

2. Mwl saving account- (ambayo ndo wengi tunayo).

3. Fixed deposits.

Hii ina Aina tatu za uwekaji fedha.

A. Waweza kuweka pesa kwa miezi mitatu mitatu.
B.Waweza kuweka kwa miezi sita sita
C. Waweza kuweka kwa mwaka.

Interest inayotokana na uwekaji wa fedha hizi mteja anaweza kuichukua mwanzoni au anaweza kuhitaji aipate kila mwezi pia anaweza kuichukua mwishoni mwa kipindi husika ikiwa na principal yake.

4. Tukutane January(ni Aina ya saving account).

Hii hutumika kama kibubu.unaweka fedha wakati wowote Ila huruhusiwi kuichukua hadi January au February. Ni kwaajili ya kushughulikia changamoto za ada na Kodi ya nyumba.

KUNA CHANGAMOTO KIDOGO:

1. Baadhi ya walimu / wateja wanashindwa kutofautiana kati ya bank na CWT.

Bank ni chombo kinachojiendesha chenye waajiriwa wanaoongozwa na masharti/maelekezo ya Bank kuu.

Faida inayopaswa kuonekana ni kwamba chama kinawahamasisha walimu wafungue account tu, na Hata ikiwezekana wapitishe mishahara huko ili mzunguko wa fedha uwe mkubwa Hatimaye wenye hisa wafikie hatua ya kugawana faida.

Pili, walimu wanashindwa kutofautisha kati ya Hisa walizonunuliwa kama wamiliki wa bank.

Na kwamba Hisa si fedha ambayo kila mtu amewekewa kwenye account na kwamba ipo MCB bank. Hisa ni kitu kungine.


MAMBO MENGINE MUHIMU YALIYOWAFANYA WALIMU WAMIMINIKE ZAIDI KWENYE BANK YAO.

Naomba tukumbuke kuwa kulikuwa na uvumi kuwa bank ya walimu huenda imo ktk orodha ya bank zilizotazamiwa kufungwa. Baada ya kusubiri kwa muda mrefu wakagundu kumbe haimo.

Pili kuwepo kwa wapotoshaji kuwa bank ya walimu ni kiini macho si ya walimu. Walimu ktk hili wamefuatilia kwa umakini mkubwa takwimu na kuona uhalisia wake kuwa hii ni miongoni mwa bank zinazofanya vizuri.

Sasa kuna kitu wamejifunza kama ifuatavyo:

Kwanza, kila anayekwenda kuomba mkopo anaelezwa vizuri kwa mahesabu kuwa pamoja na Kiwango anachotaka kuchukua, zipo gharama za KUANDAA MKOPO na gharama za BIMA ya mkopo zitakazokatwa kutoka ktk mkopo huo. Na hili ni kwa kila bank.

Jambo hili ktk bank nyingine halielezwi wazi kwa wateja wao ili wajue.mteja anashtukia Kiwango alichoomba kimepu ngua bila kujua.

MCB bank inamwezesha mteja ajipange kuongeza Kiwango flani ikiwezekana ili malengo yake yabaki palepale.

Bima ya mkopo inachajiwa kwaajili ya dharura kama mtu akipata ulemavu wa KUDUMU inacover na kama mtu atafariki yenyewe itahusika - familia Haitadaiwa chochote.

Pili, MCB makato yake ya gharama hizo ni ni ndogo sana ukilinganisha na bank zingine. MCB mteja anachajiwa gharama ya KUANDAA mkopo kwa 3% kutoka ktk mkopo wake ambapo bank zingine zinakata hadi 7% au 8% mahali pengine.

MCB katka gharama za BIMA ya mkopo wanakata 0.5% wakati bank zingine wanakata hadi 2% ya mkopo huo.
N.B kabla ya kuchukua mkopo ulizeni haya. Ndio utofauti uliopo kati ya bank zingine na bank ya mwl. na ndiyo faida iliyowafanya walimu WAMIMINIKE kwa wingi kwao.

ANGALIA MFANO ULIOKUWA UKIWATATIZA WALIMU WENGI:

Mf. Mwl mwenye basic salary 716,000/= na take home 516,000/=
Tuchukulie anahitaji mkopo wa sh.10,000,000/= kwa miaka 6. Atakatwa na MCB 3% ya kuandaa mkopo = sh. 300,000/= na 0.5% ambayo huchajiwa mara1 tu pesa ambayo ingechargiwa kwa kila mwezi kwa miaka sita kidogokidogo ambayo inaleta jumla ya sh. 300,000/= . Jumla kuu ya gharama zote za maandalizi ya mkopo na bima= na sh 600,000/= .

Hivyo wanapata elimu kuwa ukichukua mil 10. Utakatwa laki sita ,hivyo utapewa kiasi cha sh. Mil 9,400,000=

Na hiki ni Kiwango kidogo kinachotolewa kwenye bank ya MCB. Sehem nyingine ni zaidi ya hapo kutegemeana na percent wanazocharge.

Kwa miaka 7 na miezi miwili atachukua 9,341,500/= kwann kwa sababu kadiri miezi inavyoongezeka makato ya mtu yanapubgua hayawi makubwa.

KUMBUKENI:

Wanasisitiza kuwa kabla hujapigiwa hesabu ya mkopo MCB, kama unataka wanunue mkopo, nenda kwanza kapige hesabu kwenye bank hiyo yenye mkopo huko wakupe Baki yako halisi baada ya kuondoa interest ambazo zingechajiwa kama mkopo ungefika hadi mwisho wa miaka uliyouchukulia.
Kisha nenda MCB utapata hela yakutosha.

KUNA AINA MBILI ZA KUCHAJI RIBA:

1. Redusing balance.
Riba inayopungua kwa kila mwezi.
Hii ndiyo hutumiwa na MCB.

2.Flate rate.
Hii iko constant. Tangu mwanzo hadi mwisho haipungui.Hii husababisha kuanzia na riba kuwa kubwa mwishoni unapomalizia mkopo.

USHAURI:
Viongozi wa chama Cwt tuendelee kuwahamasisha walimu,kuwapa taarifa juu ya maboresho makubwa yaliyofanyika na bank ya MCB.

Hii itaharakisha walimu kupata faida kupitia hisa walizowekeza Hatimaye kuanza kupata gawio.

Kwa sasa ilikuwa Bado mapema kulipata kwakuwa walimu mwenyewe hawakuwa wameona umuhimu wa kuendeleza kilichochao na badala yake walikuwa wakisaidia kuzalisha faida za wawekezaji wa hisa kwenye bank zingine.kwa kupitisha mishahara na mikopo huko. (Umoja ni nguvu)

MWISHO NATOA WITO/OMBI MUHIMU:

Kwamba, ni vema Bodi ya MCB kuangalia kwa jicho la tatu kama inawezekana kupanua wigo wa ununuzi wa mikopo kuanzia mil 3 hadi mil 5.

Lengo Ni kuwafanya walimu wasiokopesheka waweze kununuliwa madeni yao na MCB bank. Ikumbukwe kuwa benki nyingi zinaishia ukomo wa kununua madeni hadi million 3 tu.


Uchambuzi na utafiti huu umefanywa
nami

MC Teacher(Mhazina Ubungo).
 
Vile nimeona paragraph ya mwanzo umeandika umetembelea tu lakini maelezo gazeti zima, basi hata sikuyasoma nikaona kama ni promo
Unisamehe tu kama sivo mawazo yangu yalipo
 
Kwahiyo, Umetembelea Tu Hapo Na Umeyapata Hayo Yote!
 
Hivi iliyounganishwa na bank ya Posta siyo hii?
 
Mleta mada.kwa kumbukumbu nilizonazo walimu wako mikoa yote Tanzania na wilaya zote Tanzania. Hii bank imejikita dar tu.mmeshindwa kuwa haya na branch popote Tanzania, Leo mnasema mnatoa mikopo kwa walimu wote wapitie eti cat huo ni uhaini.pili kila mwezi mnakata misharaha ya walimu 2% kwa lazima hizo fedhamnapeleka wapi na zinafanya kazi gani ? Leo nanakuja kuwaambia walimu mnataka kuwakopesha warudishieni kwanza fsida ya 2% mnayowaksta kila mwezi kwa miaka yote.tatu tunaomba walimu wafahamu jengo LA mwalimu house lilijenga kwa gharama gani na mapato yanayotokana na jengo hili ni sh ngapi na yanafanya kazi gani.? Mwisho kuna magari used yalinunuliwa nchi zima kwa ajili ya makatibu Wa cwt wilaya na Mkoa.swali ni nani alipitisha tenda ya kununua magari used? Je Fedha zilitoka wapi na ndani analipa huo Mkopo Wa magari used?walimu wamehamia cwt wanalipwa na ndani na kiadi gani? Hii bank ni jipu, bora walimu wabaki na nmb na Crdb yao.jumapili njema
 
ban
Hii bank ni white elephant project
 
Hii bank imetokana na michango ya walimu(cwt),nilitegemea ndio itakuwa mkombozi wao hususani riba za kinyonyaji.Inavyoonekana ni kiini macho tu ya kupiga pesa ya walimu wanyonge.USHAURI;.Riba lazima iwe single digit kwa wanachama wao kama wana nia ya dhati
 
Vile nimeona paragraph ya mwanzo umeandika umetembelea tu lakini maelezo gazeti zima, basi hata sikuyasoma nikaona kama ni promo
Unisamehe tu kama sivo mawazo yangu yalipo
Ingekuwa vyema zaidi kama ungepita kimya kimya.
 
Ni michango ya walimu.wamekatwa Fedha na riba ni kubwa.bora nmb na Crdb riba ni 17%na hakuna michango ya walimu.cwt ni chama cha kuwanyonya walimu.hii bank imeanzisjwa tena ni bank ya kuwanyonya walimu.swali mwalimu anaponea wapi? Jumapili njema
 
Wamiminika vp huku hawawezi kutofautisha CWT na MCB?
Acha kuzunguka mbuyu lipia tangazo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…