Walimu waboreshewe maslahi

mansakankanmusa

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2010
Posts
4,162
Reaction score
796
Nashangaa sana tatizi linajulikana, walimu hawana pesa, endapo watalipwa japo milioni moja tu kama cash kwa mwezi, mtashangaa.

wote wanaosemasema wanajisumbua tu. wengine wanafanya hili tatizo kama mtaji ktk siasa, endelezeni siasa tutaishia pabaya.

serikali ichukue ushauri huu, iweke pembeni mambo yote, walipeni walimu kuanzia mwezi july mshahara usiopungua mil.1

bajeti yenu izingatie tatizo la pesa kwa walimu, sote tutashangazwa na utendaji kazi wa walimu wetu.

MH. RAIS ashauriwe atumie mamlaka yake kuongeza pesa kwa walimu atakuwa ameokoa

Maoni yangu!
 
Siyo 1m, hata wakafika laki 7 ikifika tu walimu watafundisha vizuri na wanafunzi watafaulu
 
yaanikaka mupi hadi machozi yananitoka, ukweli pesa, sio madarsa na kuwajaza walimu, ni moyo wa walimu tu

walimu wetu nawajua sana ni watu wema sana ttzo ni siasa.

wakiwalipa vizuri, hata sekta hii itagombaniwa, kila mkoa wataenda. mungu tusaidie waelewe wajue ukweli
 
kuna kitu kinaitwa IMPROVIZATION walimu wawalipe kwanza, kisha watatue matatizo mengine baadae

kutanguliza matatizo bila kijali WALIMU ni kutwanga maji kwenye kinu...waelewe tatizo tutoke hapa.
 
Siyo walimu tu kuna askari, manesi, wafanyakazi wa reli,na wafanyakazi kwa ujumla
 
Serikali yetu ni serikali sikivu,,basi inaishia hapo hapo kwenye kusikia,, so tusubirie labda ikirebooot inaweza ikawa waka na driver za utendaji,,
 
ni kuboresha mshahara, madhingira ya kazi, elimu aipatayo na utendaji kazihakuna mchawi tena hapo wala uhitaji wa BRN
 
Tutatengeneza jamii ya watu ambao, watakuwa hawaajiriwi popote pale
 

!
!
uwingi wa hela sio ishu, ishu ni uwezo wa hiyo hela katika manunuzi. Tufanye wapewe milioni kumi halafu debe la mahindi likawa laki moja itasaidia nini?.. Cha msingi ni kuhakikisha mfumuko wa bei unadhibitiwa ili hata hiyo ndogo wanayoipata itosheleze mahitaji. Maji hayawezi kujaa kwenye kikapu hata siku moja.
 
Kama unaufaham wa kutosha, mwal hana posho yoyote zaid ya mshahara,

ukilinganisha na watendaji wengine wa umma wanavijisehem vya kuponea kabla ya mwishi wa mwezi, mkuu hiyo ndiyo maana yangu.

swala la inflation ni kitu kingine kwa walimu, ama unamaana wakipandishiwa mshahara ndipo inflation itaanza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…