Polite
JF-Expert Member
- Apr 12, 2011
- 1,095
- 816
Maelfu ya watoto nchini Uingereza na Wales,
wanakabiliwa na tisho la kukosa elimu huku
walimu wao wakigoma.
Walimu hao wanagoma wakitaka nyongeza ya
mishahara, malipo mazuri ya uzeeni na
kuboreshwa kwa mazingira ya kazi.
Wanachama wa chama cha walimu, (NUT)
watashiriki katika mgomo huo huku wakiacha
shule nyingi bila walimu huku masomo
yakisitishwa.
Walimu hao wamesema hawakuwa na budi ila
kuondoka kazini kwani hakuna suluhu la
matatizo yao.
Wizara ya elimu hata hivyo imelalamika ikisema kuwa mgomo huo unaathiri maisha ya wazazi na elimu kwa watoto.
Mgomo huu ulianza baada ya walimu
kukubaliana kupiga kwa kura mwezi Mei 2011
na Juni 2012.
Asilimia 92 ya walimu walipiga kura ya ndio
kwa gomo kufanyika.
Chama cha walimu nchini humo kimekuwa
kikivutana na serikali kwa miaka miwili sasa na
hata kufanya migomo midogomidogo hadi
mgomo huu mkubwa ukafikiwa.
Source BBC SWAHILI.